Tuesday, April 1, 2014

NGORONGORO HEROES KWENDA NAIROBI.

Kikosi cha watu 27 wakiwemo wachezaji na benchi la ufundi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kinatarajia kuondoka keshokutwa (Aprili 3 mwaka huu) kwenda Nairobi, Kenya.
TFF_LOGO12Ngorongoro Heroes inayofundishwa na John Simkoko ipo kambini tangu Machi 23 mwaka huu kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya (U20). Mechi hiyo ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri huo itachezwa Jumapili (Aprili 6 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini Nairobi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (Aprili 1 mwaka huu), Kocha Simkoko amesema wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, na nia ni kupata matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini wiki tatu baadaye.
Kikosi cha Ngorongoro Heroes chenye wachezaji 20 na viongozi saba kitaondoka saa 4.30 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Msafara wa timu hiyo utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi Abdoulkarim Twagiramukiza, Ambroise Hakizimana, Raymond Bwiliza na Louis Hakizimana wote kutoka Rwanda wakati Kamishna ni Maxwell Mtonga wa Malawi.
Ngorongoro Heroes itaagwa kesho (Aprili 2 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF.
MIKOA KUMI YATUMA WAWAKILISHI WAKE RCL
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kumi vimewasilisha majina ya mabingwa wao watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).
Mabingwa hao ni Arusha (AFC), Kilimanjaro (Panone FC), Lindi (Kariakoo SC), Manyara (Tanzanite SC), Mara (JKT Rwamukoma), Morogoro (Volcano FC), Mtwara (Pachoto Shooting Stars), Pwani (Kiluvya United), Shinyanga (Bulyanhulu FC), Singida (Singida United) na Tanga (African Sports).
Mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa wake ni Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Simiyu na Tabora wakati mikoa ya Dodoma na Mwanza imeomba kuongezewa muda kutokana na sababu mbalimbali.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliagiza kuwa mikoa yote iwe imemaliza ligi na kuwasilisha jina la bingwa wake Machi 30 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: DROO RAUNDI YA MCHUJO YACHUKUWA NAFASI LEO

DROO ya Raundi ya Mchujo ya Mashindanoya CAF ya Kombe la Shirikisho imefanywa Leo huko Mjini Cairo, Misri na kuibua Mechi za mvuto ikiwemo Dabi ya Jiji la Bamako huko Nchini Mali.
Droo hii ilihusisha Timu 8 zilizoshinda Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Kombe la Shirikisho na Timu 8 zilizotolewa kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Waliokuwa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri, ambao walibwagwa na Al Ahly Benghazi ya Libya kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI na kutupwa Kombe la Shirikisho, wamepangiwa kucheza na Klabu ya Morocco, Difaa El Jadida.
Dabi ya Jiji lCAF-LOGO14a Bamako, itahusisha Klabu za huko Nchini Mali, Real Bamako, iliyotokea CAF CHAMPIONZ LIGI, dhidi ya Djoliba.
Mechi za Raundi ya Mchujo zitachezwa Aprili 18 na Marudiano Wiki moja baadae na Washindi 8 wataingizwa kwenye Droo ya Makundi ambapo Makundi mawili ya Timu 4 kila moja yatapangwa.
CAF Kombe la Shirikisho
Raundi ya Mchujo
Al Ahly (Egypt) vs Difaa El Jadida (Morocco)
Real Bamako (Mali) vs Djoliba (Mali)
AC Leopards (Congo) vs Medeama (Ghana)
Kaizer Chiefs (South Africa) vs ASEC Mimosas (Cote d'Ivoire)
Coton Sport (Cameroon) vs Petro Luanda (Angola)
Horoya (Guinea) vs ES Tunis (Tunisia)
Sewe Sport (Cote d'Ivoire) vs Bayelsa United (Nigeria)
Nkana (Zambia) vs Bizertin (Tunisia).
**Mechi kuchezwa Aprili 18 na Marudiano Wiki moja baadae
**Washindi 8 kuingizwa Droo ya Kupanga Makundi mawili

UCL:KAZI IPO MAN UNITED VS BAYERN MUNICH,BARCA KUIKABIRI ATLETICO MADRID

ROBO FAINALI
Robo Fainali
Mechi za Kwanza
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumanne Aprili 1
Barcelona v Atletico Madrid
Manchester United v Bayern Munich
Leo Usiku Uwanja wa Old Trafford huko Jijini Manchester utashuhudia mtanange mkali kati ya Mabingwa wa England, Manchester United, na Mabingwa wa Ulaya, ambao pia ndio Mabingwa wa Germany, Bayern Munich, katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Mara ya mwisho kukutana kwa Timu hizi kwenye Michuano ya Ulaya ni Mwaka 2010 wakati Bayern Munich ilipoitoa Man United kwenye Robo Fainali kwa Bao za Ugenini.
Safari hii, hali ipo tofauti kwani Man United wanaingia kwenye Mechi hii huku Wachambuzi wengi hawawapi matumaini makubwa ya kufanya viziru dhidi ya Bayern Munich inayosifiwa kuwa ndio Timu Bora Ulaya hivi sasa na Juzi ilitwaa tena Ubingwa wa Germany huku wakiwa na Mechi 7 mkononi wakati Man United wanasuasua kwenye Ligi Kuu England wakiwa Nafasi ya 7.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Robo Fainali
Jumatano Aprili 2
Real Madrid v Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain v Chelsea
Marudiano
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumanne Aprili 8
Chelsea v Paris Saint-Germain
Borussia Dortmund v Real Madrid
Jumatano Aprili 9
Bayern Munich v Manchester United
Atletico Madrid v Barcelona
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU
MSHINDI
NCHI
MSHINDI WA PILI
NCHI
GOLI
2012-13
Bayern Munich
Germany
Borussia Dortmund
Germany
2-1
2011-12
Chelsea
England
Bayern Munich
Germany
1-1 (4–3)
2010-11
Barcelona
Spain
Manchester United
England
3-1
2009-10
Internazionale
Italy
Bayern Munich
Germany
2-0
2008-09
Barcelona
Spain
Manchester United
England
2-0
2007-08
Man United
England
Chelsea
England
1-1 (6–5)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
WAFUNGAJI BORA 2013/14:
C. Ronaldo-Real Madrid Goli 13
Zlatan Ibrahimovic-PSG Goli 10 [Penati 1]
Messi-Barcelona Goli 8 [Penati 2]
Diego Costa-Atletico Madrid Goli 7
Sergio Agüero-Manchester City Goli 6 [Penati 2]