Monday, July 22, 2013

PUYOL ASEMA TITO VILANOVA AMEWEKA PIGO KWA BARCA

Nahodha wa club ya Fc Barcelona, Carles Puyol amesema kuwa uamuzi wa Tito Vilanova kuachia ngazi kuinoa klabu hiyo kuwa ni pigo kubwa. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alitangaza kuachia ngazi wiki iliyopita ili zweze kuendelea na matibabu yake ya saratani baada ya kuiongoza Barcelona kunyakuwa taji la La Liga katika msimu wa 2012-2013.
Puyol amekiri kuwa habari ya kujizulu kwa Vilanova imekuja kwa mshituko lakini ameahidi kuonyesha kiwango cha hali ya juu msimu ujao ikiwa kama sehemu ya kumshukuru kocha huyo. Beki huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akisumbuliwa na majeruhi amedai kuwa wakati Vilanova akiwaaga aliwaomba kujituma kwa bidii katika msimu mpya uliopo mbele yao na watafanya hivyo kwa heshima yake.

UONGOZI WA URA YA UGANDA YAJIA JUU SIMBA KUHUSU OWINO"

URA ya Uganda kupitia uongozi wake umeamua kujajuu na kusema unashangazwa na kuiona inamtaka beki Joseph Owino.
Meneja wa URA, Sam Okabo amesema Simba walimuona mchezaji huyo hana thamani wakati akiwa mgonjwa.
Simba ilimuacha Owino ikiwa ni siku chache baada ya kubadilishana na Uhuru Selemani ambaye alikwenda Azam FC.
Lakini ikaonekana alikuwa hajapona vizuri hivyo viongozi wa Simba wakaamua kuachana naye na kuanza kuhaha kusaka mabeki wengine.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope alimfuata Owino baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya URA ambayo Msimbazi walilala.

DAVID MOYES ATHIBITISHA KUHUSU CLUB HIYO KUTUMA OFA YA PILIM KUHUSU FABRIGAS

Mrithi wa Sir Alex Ferguson Meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes amethibitisha kuwa klabu hiyo imetuma ofa nyingine kwa ajili ya kujaribu kumsajili Cesc Fabregas na kuonya kuwa bado hajakata tamaa na kiungo huyo wa Barcelona. Akihojiwa na waandishi wa habari katika Uwanja wa Nissan jijini Yokohama, Japan, Moyes amesema ofisa mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward bado anafanya mawasiliano na Barcelona kuhusiana na Fabregas baada ya kutuma ofa ya pili inayokadiriwa kufikia paundi milioni 30 ambayo itakuwa rekodi mpya ya klabu kwenye usajili. 
Moyes amedai kuwa ingawa wana wachezaji kadhaa ambao wako katika mipango yao kama usajili wa Fabregas ukishindikana lakini kwasasa bado hawajakata tamaa ya kupata saini ya nyota huyo. United kwasasa wako katika ziara yao ya tatu jijini Tokyo ambapo tayari nyota wake Shinji Kagawa, Ashley Young na Chris Smalling wameshaungana na wenzake baada ya kupona

MESSI AMPIGIA UPATU KOCHA MPYA MARTINO KUCHUKUA MIKOBA YA VILANOVA

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya argetina Lionel Messi amempigia upatu kocha Gerardo Martino kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo. Baada ya nafasi ilikuwa wazi kutokana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Tito Vilanova kulazimika kuachia ngazi kutokana na maradhi ya saratani yanayomsumbua. 
Martino ambaye aliiongoza timu ya Old Boys kushinda taji la Ligi Kuu chini Argentina msimu uliopita ni mmoja wa makocha wanaoewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Vilanova na Messi ana imani kuwa kocha huyo anastahili nafasi hiyo. Messi alidai kuwa Martino ni mmoja wa makocha wenye kiwango cha juu na kila mtu anamheshimu hivyo haoni tatizo kama akikabidhiwa mikoba ya kuinoa Barcelona.

MOURINHO AMPASHA DAVID MOYES KUSAHAU KUMNASA C.RONALDO

The spesho one Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amemhabarisha meneja wa Manchester United, David Moyes kusahau ndoto zake za kujaribu kumrejesha Cristiano Ronaldo Old Traford. Kuna tetesi kuwa United wako katika harakati za kujaribu kumrejesha nyota huyo wa kimataifa wa Ureno pamoja na meneja mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti kusisitiza kuwa hawatamuuza. Lakini Mourinho ambaye msimu uliopita alikuwa akiinoa klabu hiyo amedai kuwa hadhani kama Madrid wanaweza kumruhusu Ronaldo kuondoka kwasababu ya uwezo mkubwa wa kifedha walionao kwasasa. Mourinho amesema Madrid ni klabu tajiri duniani na hawana sababu ya kumuuza nyota huyo hivyo wanaweza kukataa ofa yoyote itakayotolewa kwa ajili ya kumchukua.

LIGI KUU YA VODACOM 2013/2014 KUANZA AGOSTI 24

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kuwa viwanjani katika miji saba tofauti.
Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha). 
Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani. (Ratiba ya mzunguko wa kwanza na wa pili imeambatanishwa- attached).

 RAUNDI YA KWANZA LIGI KUU VODACOM TZ BARA
NO DATE No.  HOME TEAM AWAY TEAM STADIUM REGION
1 24.08.2013 1 YOUNG AFRICANS ASHANTI UNITED NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  24.08.2013 2 MTIBWA SUGAR AZAM FC MANUNGU MOROGORO
  24.08.2013 3 JKT OLJORO COASTAL UNION SH. AMRI ABEID ARUSHA
  24.08.2013 4 MGAMBO JKT JKT RUVU  MKWAKWANI TANGA
  24.08.2013 5 RHINO RANGERS SIMBA SC A.H. MWINYI TABORA
  24.08.2013 6 MBEYA CITY KAGERA SUGAR SOKOINE MBEYA
  24.08.2013 7 RUVU SHOOTINGS TANZANIA PRISONS MABATINI PWANI
 
2 28.08.2013 8 MTIBWA SUGAR KAGERA SUGAR MANUNGU MOROGORO
  28.08.2013 9 RHINO RANGERS AZAM FC A.H. MWINYI TABORA
  28.08.2013 10 JKT RUVU TANZANIA PRISONS MABATINI PWANI
  28.08.2013 11 MBEYA CITY RUVU SHOOTINGS SOKOINE MBEYA
  28.08.2013 12 MGAMBO JKT ASHANTI UNITED MKWAKWANI TANGA
  28.08.2013 13 JKT OLJORO SIMBA SC SH. AMRI ABEID ARUSHA
  28.08.2013 14 YOUNG AFRICANS COASTAL UNION NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
(29.August-09.Sept. National Team Camp for WCQ against Gambia away)
3 14.09.2013 15 SIMBA SC MTIBWA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  14.09.2013 16 COASTAL UNION TANZANIA PRISONS MKWAKWANI TANGA
  14.09.2013 17 RUVU SHOOTINGS MGAMBO JKT MABATINI  PWANI
  14.09.2013 18 JKT OLJORO RHINO RANGERS SH. AMRI ABEID ARUSHA
  14.09.2013 19 MBEYA CITY YOUNG AFRICANS SOKOINE MBEYA
  14.09.2013 20 KAGERA SUGAR AZAM FC KAITABA KAGERA
  14.09.2013 21 ASHANTI UNITED JKT RUVU AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM


4 18.09.2013 22 TANZANIA PRISONS YOUNG AFRICANS SOKOINE MBEYA
  18.09.2013 23 SIMBA SC MGAMBO JKT NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  18.09.2013 24 KAGERA SUGAR  JKT OLJORO KAITABA KAGERA
  18.09.2013 25 AZAM FC ASHANTI UNITED AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  18.09.2013 26 COASTAL UNION RHINO RANGERS MKWAKWANI TANGA
  18.09.2013 27 MTIBWA SUGAR MBEYA CITY MANUNGU MOROGORO
  18.09.2013 28 RUVU SHOOTINGS JKT RUVU MABATINI PWANI
 
5 21.09.2013 29 MGAMBO JKT RHINO RANGERS MKWAKWANI  TANGA
  21.09.2013 30 TANZANIA PRISONS MTIBWA SUGAR SOKOINE MBEYA
  22.09.2013 31 JKT RUVU JKT OLJORO AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  21.09.2013 32 SIMBA SC MBEYA CITY NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  22.09.2013 33 AZAM FC YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  21.09.2013 34 KAGERA SUGAR ASHANTI UNITED KAITABA KAGERA
  22.09.2013 35 COASTAL UNION RUVU SHOOTINGS MKWAKWANI  TANGA
     
6 28.09.2013 36 YOUNG AFRICANS RUVU SHOOTINGS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  28.09.2013 37 RHINO RANGERS KAGERA SUGAR A. H. MWINYI TABORA
  29.09.2013 38 ASHANTI UNITED MTIBWA SUGAR AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  28.09.2013 39 MBEYA CITY COASTAL UNION SOKOINE MBEYA
  28.09.2013 40 MGAMBO JKT JKT OLJORO MKWAKWANI TANGA
  29.09.2013 41 JKT RUVU SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  29.09.2013 42 TANZANIA PRISONS AZAM FC SOKOINE MBEYA
 
7 05.10.2013 43 RUVU SHOOTINGS SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES  SALAAM
  05.10.2013 44 JKT RUVU KAGERA SUGAR AZAM COMPLEX DAR ES  SALAAM
  05.10.2013 45 COASTAL UNION AZAM FC MKWAKWANI TANGA
  05.10.2013 46 JKT OLJORO MBEYA CITY SH. AMRI ABEID ARUSHA
  25.09.2013 47 RHINO RANGERS ASHANTI UNITED A. H. MWINYI TABORA
  06.10.2013 48 MGAMBO JKT  TANZANIA PRISONS MKWAKWANI TANGA
  06.10.2013 49 YOUNG AFRICANS MTIBWA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES  SALAAM
 
8 09.10.2013 50 RHINO RANGERS MBEYA CITY A. H. MWINYI TABORA
  09.10.2013 51 JKT OLJORO RUVU SHOOTINGS SH. AMRI ABEID ARUSHA
  09.10.2013 52 AZAM FC MGAMBO JKT AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  09.10.2013 53 MTIBWA SUGAR JKT RUVU MANUNGU MOROGORO
  12.10.2013 54 KAGERA SUGAR YOUNG AFRICANS KAITABA KAGERA
  12.10.2013 55 SIMBA SC TANZANIA PRISONS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  13.10.2013 56 ASHANTI UNITED COASTAL UNION AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
     
9 13.10.2013 57 RUVU SHOOTINGS RHINO RANGERS MABATINI PWANI
  13.10.2013 58 MGAMBO JKT MBEYA CITY MKWAKWANI TANGA
  13.10.2013 59 AZAM FC JKT RUVU AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  13.10.2013 60 MTIBWA SUGAR JKT OLJORO MANUNGU MOROGORO
  16.10.2013 61 ASHANTI UNITED TANZANIA PRISONS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  19.10.2013 62 KAGERA SUGAR COASTAL UNION KAITABA KAGERA
  20.10.2013 63 SIMBA SC  YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 
10 19.10.2013 64 JKT OLJORO AZAM FC SH. AMRI ABEID ARUSHA
  19.10.2013 65 MTIBWA SUGAR MGAMBO JKT MANUNGU MOROGORO
  19.10.2013 66 MBEYA CITY JKT RUVU SOKOINE MBEYA
  19.10.2013 67 ASHANTI UNITED RUVU SHOOTINGS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  23.10.2013 68 COASTAL UNION SIMBA SC MKWAKWANI TANGA
  23.10.2013 69 TANZANIA PRISONS KAGERA SUGAR SOKOINE MBEYA
  23.10.2013 70 YOUNG AFRICANS RHINO RANGERS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 
11 26.10.2013 71 TANZANIA PRISONS MBEYA CITY SOKOINE MBEYA
  26.10.2013 72 COASTAL UNION MTIBWA SUGAR MKWAKWANI TANGA
  26.10.2013 73 JKT OLJORO ASHANTI UNITED SH. AMRI ABEID ARUSHA
  26.10.2013 74 YOUNG AFRICANS MGAMBO JKT NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  27.10.2013 75 RUVU SHOOTINGS  KAGERA SUGAR MABATINI PWANI
  27.10.2013 76 SIMBA SC AZAM FC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  27.10.2013 77 RHINO RANGERS JKT RUVU A. H. MWINYI TABORA
 
12 30.10.2013 78 MGAMBO JKT  COASTAL UNION MKWAKWANI TANGA
  30.10.2013 79 TANZANIA PRISONS JKT OLJORO SOKOINE  MBEYA
  30.10.2013 80 AZAM FC RUVU SHOOTINGS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  30.10.2013 81 SIMBA SC KAGERA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  30.10.2013 82 MTIBWA SUGAR RHINO RANGERS MANUNGU MOROGORO
  30.10.2013 83 MBEYA CITY ASHANTI UNITED SOKOINE  MBEYA
  31.10.2013 84 JKT RUVU YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 
13 02.11.2013 85 JKT RUVU COASTAL UNION AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  02.11.2013 86 ASHANTI UNITED SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
  03.11.2013 87 KAGERA SUGAR MGAMBO JKT KAITABA KAGERA
  03.11.2013 88 AZAM FC MBEYA CITY AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
  03.11.2013 89 RHINO RANGERS TANZANIA PRISONS A. H. MWINYI TABORA
  03.11.2013 90 RUVU SHOOTINGS MTIBWA SUGAR MABATINI PWANI
  03.11.2013 91 YOUNG AFRICANS JKT OLJORO NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAML 
             








TAIFA STARS KWENDA KAMPALA J5
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.

Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)