Wednesday, April 23, 2014

MTIBWA IPO MBIONI KUTOLEA MACHO WANANDINGA WAPYA

Timu ya soka ya Mtibwa Sugar Mabingwa wa zamani wa Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000wamekiri kukumbana na changamoto kubwa msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu Tanzania bara uliomalizika aprili 19 mwaka huu .
 Afisha habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru Lugalambwike ameueleza mtandao huu kuwa kitu kikubwa walichojifunza ni maandalizi makubwa ya baaadhi ya timu zinazoshiriki ligi kuu toafuti na wao.
“Sisi ni wakongwe katika ligi hii, lakini tumeshindwa kuonesha cheche kutokana na kuwepo kwa timu zenye kiwango kizuri. Mbeya City fc wametikisa kweli, sio kwetu tu hata Simba na Yanga wamekumbana na upinzani na ndio maana wamekosa ubingwa ”.
“Kikubwa tumebaini changamoto zetu ikiwemo kukosa wachezaji muhimu kikosini. Tunataka kufanya usajili mzuri ili tuanze maandalizi ya mapema”.

BURUNDI KUTUA KESHO NCHINI KUIKABILI STARS

Timu ya Taifa ya Burundi (Intamba Mu Rugamba) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Intamba Mu Rugamba it
Burundi-CECAFA-Teamakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 jioni
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

MALINZI AWAPA PONGEZI SUKER, LEKJAA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza marais Davor Suker na Fouzi Lekjaa kwa kuchaguliwa tena hivi karibuni kuongoza mashirikisho ya mpira wa miguu katika nchi zao.
Suker amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Croatia (CFF) wakati Lekjaa amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRFM).
Katika salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amesema ushindi waliopata ni uthibitisho kuwa familia ya mpira wa miguu katika nchi zao ina imani kubwa kwao katika kuendeleza mchezo huo ndani na nje ya nchi hizo.
Rais Malinzi amesema Lekjaa na Suker wana uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari imefanyika, lakini vilevile kuja na mawazo mapya ambayo yatakuwa changamoto kwa ustawi wa mchezo huo nchini Morocco na Croatia kwa ujumla.