Timu ya soka ya Mtibwa Sugar Mabingwa
wa zamani wa Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000wamekiri
kukumbana na changamoto kubwa msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu Tanzania
bara uliomalizika aprili 19 mwaka huu .
“Sisi
ni wakongwe katika ligi hii, lakini tumeshindwa kuonesha cheche
kutokana na kuwepo kwa timu zenye kiwango kizuri. Mbeya City fc
wametikisa kweli, sio kwetu tu hata Simba na Yanga wamekumbana na
upinzani na ndio maana wamekosa ubingwa ”.
“Kikubwa
tumebaini changamoto zetu ikiwemo kukosa wachezaji muhimu kikosini.
Tunataka kufanya usajili mzuri ili tuanze maandalizi ya mapema”.