Monday, November 3, 2014
SUMATRA MKOA WA MBRYA YASEMA HATAVUMILIA TABIA ZA MADERA KUJAZA MAFUTA WAKATI WA KUBEBA ABIRIA.
MAMLAKA ya usafiri na udhibiti wa nchi kavu na majini (Sumatra)
mkoa wa Mbeya imesema kuwa haitavumilia tabia ya baadhi ya watumiaji wa vyombo
vya usafiri kujaza mafuta wakati vikiwa vimebeba abiria.
Aidha mamlaka hiyo imesisitiza kuwa ikiwa watumiaji hao
watabainika kutenda kosa hilo watatozwa faini ya shilingi laki mbili na nusu.
Akizungumza na Highlands fm, Afisa mfawidhi wa Sumatra, Denis Daud
amesema vitendo hivyo vinahatarisha usalama wa abiria na
kwamba mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa watumiaji hao.
Katika hatua nyingine Daud, amewataka watumiaji hao kujaza mafuta
ya kutosha kwenye magari yao ili kuondoa usumbufu kwa abiria pindi magari hayo
yanapokata mafuta barabarani.
MAKONDA AKANUSHA KUMPIGA MZEE WARIOBA NA KULAANI VIKALI WALIOANZISHA VURUGU,
Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha vitu alivyokwenda navyo kwenye mdahalo huo ambavyo ni katiba ya sasa na katiba pendekezwa kwa ajili ya kutumia kujibu hoja mbalimbali wakati wa mdahalo huo.
Makonda amelaani na kukanusha kuwa hakumpiga Mzee Warioba isipokuwa alikuwa na kazi moja ya kuhakikisha anamsaidia Anold Kayanda mwandishi wa BBC ambaye aliumizwa katika vurugu hizo na Mzee Warioba na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba asiyeona Amon Mpanju wakati wa vurugu zilizotokea katika mdahalo wa kujadili rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam.
Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi.
Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo
MWAKIBINGA AONDOKA BODI YA LIGI
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na TPLB wanamshukuru Mwakibinga kwa mchango wake kwa kipindi ambacho ameitumikia Bodi, na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.
TPLB hivi sasa iko katika mchakato wa kupata Ofisa Mtendaji Mkuu mpya kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mwakibinga baada ya muda wa mkataba wake kumalizika.
KOCHA NOOIJ KUTAJA KIKOSI STARS
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Subscribe to:
Posts (Atom)