Sunday, April 27, 2014

AFCON 2015-MOROCCO: DROO YAWEKWA HADHARANI

DROO ya Mashindano ya Mataifa ya Africa, rasmi kama Orange Africa Cup of Nations Morocco 2015, ambayo Fainali zake zitachezwa huko Morocco kati ya Tarehe 17 Januari hadi 8 Februari 2015, imefanyika hii Leo huko Cairo, Egypt.
Nchi 51 zitashiriki Mashindano haya ambapo Mauritania na South Sudan zilishinda toka Raundi ya Kwanza na kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano ambayo Tanzania itacheza na Zimbabwe.
AFCON_2015_LOGO-MOROCCOWashindi 14 wa Raundi ya Pili ya Mtoano wataingia Raundi ya Tatu ya Mtoano ili kupata Timu 7 zitakazosonga kwenye Makundi ambayo hii Leo pia yamepangwa.
Ikiwa Tanzania itaitoa Zimbabwe basi kwenye Raundi ya Tatu ya Mtoano itacheza na Mshindi kati ya Mozambique na South Sudan na Tanzania ikipita hapo itaingia 
KUNDI F ambako ziko Zambia, Cape Verde na Niger.
Yapo Makundi 7 ambapo Mshindi wa Kila Kundi na Mshindi wa Pili wa Kila Kundi pamoja na Timu moja iliyofuzu Nafasi ya 3 Bora katika Makundi ndizo zitaingia Fainali kuungana na Morocco na kufanya idadi ya Timu 16 kwenye Fainali.
RATIBA/MAKUNDI:
Nchi ambazo zimeingia Makundi moja kwa moja: Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Zambia, Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria, Angola, Cape Verde, Togo, Egypt, South Africa, Cameroon, DR Congo, Ethiopia, Gabon, Niger, Guinea, Senegal and Sudan.
RAUNDI YA PILI YA MTOANO

Mechi Na 1: Liberia vs Lesotho

Mechi Na 2: Kenya vs Comoros
Mechi Na 3: Madagascar vs Uganda
Mechi Na 4: Mauritania vs Equatorial Guinea
Mechi Na 5: Namibia vs Congo
Mechi Na 6: Libya vs Rwanda
Mechi Na 7: Burundi vs Botswana
Mechi Na 8: Central African Republic vs Guinea Bissau
Mechi Na 9: Swaziland vs Sierra Leone
Mechi Na 10: Gambia vs Seychelles 
Mechi Na 11: Sao Tome e Principe vs Benin
Mechi Na 12: Malawi vs Chad
Mechi Na 13: Tanzania vs Zimbabwe
Mechi Na 14: Mozambique vs South Sudan

**Mechi za Kwanza 16,17,18 Mei 2014

**Mechi za Marudiano 30,31 Mei au 1 Jun1 2014

RAUNDI YA TATU YA MTOANO
**WASHINDI 14 wa Raundi ya Pili ya Mtoano watacheza Raundi hii
TIMU MECHI NA TIMU Mechi ya Kwanza Mechi ya Pili
Mshindi Mechi Na 1 1/2 Mshindi Mechi Na 2 18–20 Julai 1–3 Agosti
Mshindi Mechi Na 3 3/4 Mshindi Mechi Na 4 18–20 Julai 1–3 Agosti
Mshindi Mechi Na 5 5/6 Mshindi Mechi Na 6 18–20 Julai 1–3 Agosti
Mshindi Mechi Na 7 7/8 Mshindi Mechi Na 8 18–20 Julai 1–3 Agosti
Mshindi Mechi Na 9 9/10 Mshindi Mechi Na 10 18–20 Julai 1–3 Agosti
Mshindi Mechi Na 11 11/12 Mshindi Mechi Na 12 18–20 Julai 1–3 Agosti
Mshindi Mechi Na 13 13/14 Mshindi Mechi Na 14 18–20 Julai 1–3 Agosti
MAKUNDI:
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi 5/6
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi 11/12
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi 1/2
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi 9/10
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi 3/4
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi 13/14
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi 7/8

TANZANIA YAITWANGA KENYA U20 KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA

TIMU ya soka ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeitoa Kenya katika Raundi ya Kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Senegal kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya bila kufungana nyumbani na ugenini.
Kwa matokeo hayo, Ngorongoro inayofundishwa na kocha mzalendo John Simkoko sasa itamenyana na Nigeria katika hatua inayofuata.
Penalti za Tanzania zilikwamishwa nyavuni na Mohammed Hussein, Kevin Friday, Mange Chagula na Iddi Suleiman, wak
ati Mudathir Yahya alikosa.
Penalti za Kenya zilifungwa na Geoffrey Shiveka, Timonah Wanyonyi na Victor Ndinya, wakati Evans Makari na Harison Nzivo walipoteza.
Hakuna kipa aliyeokoa penalti bali wapigaji waliokosa walipiga nje.
Ilikuwa mechi kali na ya ushindani na makipa wa timu zote mbili, Aishi Manula wa Tanzania na Farouk Shikhalo wa Kenya aliyeanza kabla ya kumpisha Boniface Barasa dakika ya 88 walifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo ya hatari.

MART NOOIJ AONGEZA 9 TAIFA STARS, KUIVAA MALAWI HUKO MBEYA!!

Kocha mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij ameongeza wachezaji tisa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi (The Flames) itakayochezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Martinus_Ignatius_Maria_maarufu_kama_Mart_Nooij
Naye beki Kelvin Yondani wa Yanga ambaye aliitwa awali ameondolewa katika kikosi hicho kwa vile ameshindwa kuripoti kambini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Pemium Lager inaingia kambini kesho (Aprili 28 mwaka huu) jijini Mbeya kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi.
Wakati huo huo, Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Zimbabwe katika raundi ya pili ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Stars itaanzia nyumbani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Mei 16 na 18 wakati ile ya marudiano itachezwa Harare kati ya Mei 30 na Juni 1 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)