Saturday, August 16, 2014

MAN UNITED YAPOLEA KIPONDO NYUMBANI 2-1 SWANSEA CITY

MENEJA mpya wa klabu ya Manchester United ameanza vibaya kampeni zake za Ligi Kuu baada ya kushuhudia kikosi chake kikitandikwa mabao 2-1 dhidi ya Swansea city katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Old Trafford mchana wa leo.
Wageni Swansea ndio waliokuwa wa kwanza kuchukuliwa wavu wa United kwa bao lililofungwa na Ki Sung-yueng katika dakika ya 28 lakini bao hilo lilisawazishwa muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili kupitia kwa nahodha wake Wayne Rooney.
Swansea walifunga bao lao la ushindi katika dakika ya 72 kupitia kwa Gyfi Sigurdsson hivyo kuifanya timu hiyo kupoteza mchezo wake wa ufunguzi nyumbani kwa mara ya kwanza toka mwaka 1972.
United walionekana kushindwa kabisa kutengeneza mipango ya kusawazisha bao hilo hatua ambayo mashabiki wake walionnekana kukata tamaa na kuanza kuondoka mapema uwanjani kabla ya mchezo kumalizika.
 Mashabiki wa United duniani kote kabla ya mchezo walionekana kuwa na imani kubwa na kikosi chao toka alipotua Van Gaal akichukua mikoba ya David Moyes ambaye alifanikiwa kushinda mechi zake zote za kirafiki alizocheza.

AZAM FC YAIFUMUA 4-1 ADAMA CITY KOMBE LA KAGAME CUP



Mabingwa wa tanzania bara 2013-2014 azam fc imekamilisha hayau ya makundi imemaliza katika klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuichalaza mabao 4-1 Adama City ya Ethiopia Uwanja wa Nyamirambo mjini hapa.

Kwa matokeo hayo Azam
FC ya Tanzania Bara, imekwea kileleni mwa Kundi A kwa kufikisha pointi nane baada ya mechi nne, ikishinda mbili na sare mbili na hatimaye kutinga hatua ya bRobo Fainali.

Dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupitia kwa Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ akiunganisha krosi ya Khamis Mcha ‘Vialli’ kabla ya Desaleny Debesh kuisawazishia Adama dakika ya 39.

Refa Mohamed Hassan kutoka Somalia alikataa bao la Kipre Herman Tchetche dakika ya 42, akidai kipa alibughudhiwa na kipindi cha pili Azam iliingia na moto mkali
na kufanikiwa kuongeza mabao matatu.

Kocha Mcameroon Joseph Marous Omog alifurahia matokeo hayo na akasema sasa anajipanga kwa Robo Fainali.
Kikosi cha Azam FC; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Gardiel Michael/Said Mourad dk51, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’/Farid Mussa dk61, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Mudathir Yahya dk72, John Bocco ‘Adebayor’, Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche.

MAXIMO ATOA NENO KWA PATRIC PHIRI KUHUSU VPL SEPT 20

Mbrazil Marcio Maximo Kocha Mkuu wa klabu Yanga ametoa ya moyoni kwa kumkaribisha nchini kocha wa Simba Timu pinzani wa jadi, Mzambia, Patrik Phiri aliyetua hivi karibuni na kuanza kazi ya kukinoa kikosi cha Wanamsimbazi.
Maximo alichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm huku Phiri akiwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba baada ya kuchukua mikoba iliyoachwa na  Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyetimuliwa Jumapili iliyopita.
Katikamkutano na waandishi wa habari, Maximo amesema kuwa amemkaribisha kocha huyo ambaye anafahamu kuwa ni mzuri lakini amemtaka kutambua ushindani uliopo wa ligi ya Tanzania.
Maximo amesema napenda kumwambia kocha mpya wa Simba (Patrick Phiri),  karibu Tanzania lakini ajue kuwa ligi ina ushindani wa hali ya juu japo natambua kuwa yeye ni kocha mzuri na anayeifahamu ligi ya hapa”, alisema Maximo.
Phiri ametua nchini siku chache zilizopita na kusaini mkataba wa mwaka
mmoja kuinoa Simba, hii ikiwa ni mara ya tatu tofauti kuionoa timu hiyo.
Kwa upande mwingine, Maximo alisema kuwa kikosi chake kinaendelea vizuri na mazoezi ambapo kinamchanganyiko wa vijana na wakongwe ambao wengine walikuwa kwenye timu zao za Taifa.
Maximo aliongeza kuwa beki aliyesajiliwa na timu hiyo, Edward Charles ni mchezaji mzuri anayeamini ataisaidia Yanga kwa muda mrefu kutokana na umri  wake kuwa mdogo.
Maximo anatarajia kutaja majina ya wachezaji ataokwenda nao kwenye kambi kisiwani Pemba na watakaa huko kwa takribani siku kumi na baadae kurudi Dar tayari kwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.