Monday, August 12, 2013

LOPEZ AONYESHA KIWANGO CHA JUU ZAIDI KATIKA NAFASI YAKE"

Kipa mahiri wa Real Madrid Diego López ameweka katika wakati mgumu  kocha wake Carlo Ancelotti.   
Ancelotti anaonekana kuingia katika wakati mgumu kutokana na namna Lopez kuonyesha kiwango cha juu.
 
Lopez ameonyesha kiwango cha juu katika mechi za kirafiki za timu hiyo ambazo imecheza.


Hali inayomfanya Ancelotti azidi kuchanganyikiwa kuwa yupi hasa awe kipa namba moja kati ya hao wawili.
Lopez alianza kupata nafasi ya kudaka baada ya kocha wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho kukorofishana na Casillas.


KOCHA MPYA WA BARCA ASEMA BADO KIKOSI CHANGU HAKIJA KIDHI HITAJI LANGU

Meneja mpya Barcelona, Gerardo Martino amekiri kuwa kikosi chake bado hakijawa katika hali anayoitaka.
“Kweli tumecheza na kushinda katika mechi za majaribio, lakini kiwango haikuwa kizuri.
“Hata mashabiki waliokuja katika mechi zetu watakubaliana nasi kwamba hatukuwa katika fomu nzuri.  
“Lakini tutajipanga, mambo yatakuwa tifauti tutakapoanza msimu na mechi yetu na Levante hakika tutafanya vizuri sana,” alisema kocha huyo maarufu Tata.
Kocha huyo amechukua nafasi ya Tito Vilanova ambaye ameshindwa kuendelea na kazi kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa.

AZAM FC YAMALIZA ZIARA YAKE NCHINI AFRIKA KUSINI KWA KIPONDO

Kikosi kabambe cha azam fc
Washindi wa pili mfululizo wa ligi kuu vodacom tanzania bara Azam FC leo imekamilisha ziara yake ya Afrika Kusini kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Moroka Swallows katika dimba la Uwanja wa Volkswagen Dobsonville mjini Soweto.
 
Aidha Katika Ziara hiyo huo unakuwa mchezo wao wa tatu kuambulia kipigo baada ya awali kuchapwa 3-0 na Kaizer Chiefs, 2-1 na Orlando Pirates.

Hata hivyo katika ziara hiyo wanarambaramba hao wamefanikiwa kuibuka na ushindi mchezo mmoja dhidi ya Mamelodi Sundowns baada ya kuichalaza bao 1-0. 

NADAL ATWAA TAJI LA MICHUANO YA KOMBE LA ROGER

Mchezaji tenisi nyota Rafael Nadal amefanikiwa kutawadhwa bingwa mpya wa michuano ya Kombe la Rogers baada ya kugaragaza Milos Raonic wa Canada. Nadal mwenye umri wa miaka 27 kutoka Hispania alitumia dakika 68 pekee kushinda mchezo huo kwa 6-2 6-2 na kunyakuwa taji lake la nane kwa mwaka huu. Toka arejee tena uwanjani Februari mwaka huu baada ya kupona majeraha, Nadal amefanikiwa kushinda michezo 48 kati ya 51 aliyocheza na kufanikiwa kushinda taji lake la nane katika michuano ya wazi ya Ufaransa. Kwa upande wa wanawake mwanadada anayeshika namba moja katika orodha za ubora Serena Williams wa Marekani naye alifanikiwa taji la michuano hiyo kwa kumgaragaza Sorana Cirstea wa Romania. Williams mwenye umri wa miaka 31 alihitaji dakika 65 pekee kummaliza mpinzani wake kwa 6-2 6-0 na kunyakuwa taji hilo kwa mara ya tatu.

TOURE YAYA ATWAA UCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA ASILIMIA 32%

YaYa Toure kiungo mahiri wa kimataifa wa Ivory Coast  na club ya man city ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo katika msimu wa 2012-2013 baada ya kupata asilimia 32 ya kura zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo na watumiaji wa mtandao. Toure mwenye umri wa miaka 30 anayecheza katika klabu ya Manchester City anafuatia na mshambuliaji nyota wan chi hiyo Didier Drogba aliyepata asilimia 24 wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Bony Wilfried aliyepata asilimia 17. Wengine ni Aroune Kone ambaye amejiunga na timu ya Everton akitokea Wigan mwezi uliopita pamoja na Gervino aliyejiunga na AS Roma akitokea Arsenal ambao wote kwa pamoja wamepata asilimia 15 ya kura zilizopigwa. Hiyo inakuwa mara ya tatu Toure kushinda tuzo hiyo mara nyingine ikiwa mwaka 2008 na 2009.

LIVERPOOL YAIKINGIA KIFUA BARCA KUHUSU AGGER

Wakala wa beki mahiri wa club ya Liverpool, Daniel Agger amesema kuwa Liverpool imeitupilia mbali ofa iliyotumwa na Barcelona kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo. Barcelona imekuwa ikihusishwa na kutaka kusajili mabeki kadhaa wa Ligi Kuu nchini Uingereza ambapo tayari walishatoa kitita cha euro milioni 25 kwa ajili ya beki wa Chelsea David Luiz. Chelsea waliweka wazi kuwa mabingwa wa soka nchini Hispania wanapoteza muda wao na sasa wakala wa Agger aitwaye Per Steffensen naye amebainisha kuwa Liverpool tayari wamepiga chini ofa hiyo. Wakala huyo amesema mteja wake bado ana mkataba wa miaka mitatu na Liverpool hivyo ni juu ya makubaliano ya klabu hizo mbili kuhusu ada ya uhamisho.

MAKOCHA 32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA

Makocha 32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki kozi ya Copa Coca-Cola inayoanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA).

Kozi hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre na washiriki wote tayari wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo kutoka Mauritius.


Washiriki wa kozi hiyo ni Ahazi Ibrahim Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu), Bakari Khamis Kilambo (Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura (Kagera), Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel Kapurata (Rukwa).


Faki Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba), Hamisi Omary Mabo (Kigoma), Hussein Maulid (Morogoro), Issa Lugaza (Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo Jackson Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na Kessy Juma Abdallah (Tanga).


Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Abdallah Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke),  Pius Kamande (Rukwa), Ramadhan Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan Salum Mnyoti (Manyara), Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Edgar Maokola (Ilala), Shaweji Nawanda (Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).


Fainali za U15 Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

 SEMINA YA MAKAMISHNA YAANZA DAR, MWANZA
Semina kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa  waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa 2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza.


Mafunzo hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.


Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


Kituo cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.


Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.


Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)