
i 23 mwaka huu).
Mikoa ambayo timu zake tayari zina
tiketi za robo fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin ni
Ilala, Kigoma, Mwanza, Pwani, Tanga na Temeke.
Matokeo ya mechi za leo kati ya Iringa
na Ruvuma, na ile kati ya Mbeya na Katavi ndiyo yatakayoamua ni timu zipi mbili
kati ya hizo zinakwenda Dar es Salaam kucheza robo fainali.
Timu zote zilizofuzu hatua ya robo
fainali zinatakiwa kuripoti Dar es Salaam keshokutwa (Januari 25 mwaka huu).
Fainali ya michuano hiyo itachezwa Februari Mosi mwaka huu.
TIMU YA BEACH SOCCER ZANZBAR YAWASILI DAR
Timu ya beach soccer ya Zanzibar
imewasili Dar es Salaam leo mchana, tayari kwa kambi ya pamoja na Tanzania Bara
kwa ajili ya kuunda kikosi cha Tanzania kitakashiriki mechi za mchujo za
michuano ya Afrika.
Tanzania imepangwa kucheza mechi ya
kwanza ya raundi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayofanyika kati ya Februari 13 na
15 mwaka huu jijini Mombasa. Mechi ya marudiano itachezwa wiki moja baadaye
nchini.
Zanzibar imewasili na kikosi cha
wachezaji 14 na viongozi watatu ambacho kitaungana na kile cha Tanzania Bara.
Timu hizo zitacheza jumla ya mechi nane kwenye ufukwe wa Escape One uliopo
Mikocheni, Dar es Salaam.
Mechi hizo zitachezwa mbili asubuhi na
mbili jioni kesho (Januari 24 mwaka huu), na nyingine nne kwa utaratibu huo huo
keshokutwa (Januari 25 mwaka huu) kabla ya Kocha John Mwansasu kutaja kikosi
cha mwisho Januari 26 mwaka huu.
VPL KUTIMUA VUMBI WIKIENDI
Mechi za Jumapili ni kati ya Azam na
Simba (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar na Ndanda (Uwanja wa CCM Kirumba), Stand
United na Coastal Union (Uwanja wa Kambarage),, Mbeya City na Tanzania Prisons
(Uwanja wa Sokoine), Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar (uwanja wa Mabatini), na JKT
Ruvu na Mgambo Shooting (Uwanja wa Azam Complex).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)