Tuesday, March 18, 2014

DROGBA KUFUMUA NYASI STAMFORD BRIDGE.

Mshambuliaji Mahiri wa Galatasaray ya Uturuki, akiwa na wenzake amefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge unaotumiwa na Chelsea. 
Mara tu baada ya mazoezi, Drogba amesema yuko tayari kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya kikosi hicho cha Jose Mourinho katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Nimerudi tena hapa, kwangu ni sehemu bora na yenye kumbukumbu nyingi sana. Lakini kama ni mechi, niko tayari," alisema Drogba.
Katika mechi ya kwanza jijini Istambul, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Hivyo jibu litatapikana leo.
UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

RATIBA

MARUDIANO

[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]

[Saa za Bongo]

Jumanne Machi 18

22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]

22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]

Jumatano Machi 19

22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]

22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

31 WAITWA NGORONGORO HEROES KUIKABILI KENYA.

Wachezaji 31 wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Senegal.
Ngorongoro Heroes itakayokuwa chini ya Kaimu Kocha John Simkoko akisaidiwa na Mohamed Ayoub inaingia kambini kesho (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayochezwa kati ya Aprili 4-6 jijini Nairobi.
Kikosi kinachounda timu hiyo ambayo itarudiana na Kenya kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke), Manyika Peter Manyika (Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende, Zanzibar).
Mabeki wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union), Edward Charles (JKT Ruvu), Frank Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel Gadiel Michael (Azam), Hussein Mkongo (Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed (Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani (Majimaji).
Viungo ni Ally Nassoro (Coastal Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa (Azam), Hamid Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti United), Mohamed Issa Juma (Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin (Scouting- Kinondoni), Seleman Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John (Scouting- Mwanza).
Washambuliaji ni Ally Salum Kabunda (Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto, Zanzibar), Jafari Mwambusi (Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal (Mlale JKT), Salum Abdilah Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania Prisons).

YANGA, AZAM KUUMANA VPL TAIFA

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Machi 19 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Azam itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari maalumu kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa.
Baada ya saa 6 mchana mauzo yote yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi kuanzia saa 7.30 mchana.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 7,000.
Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ambapo atasaidiwa na Anold Bugado (Singida), Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam). Kamishna wa mechi hiyo Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza.
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
19
12
7
0
27
43
2
Yanga SC
18
11
6
1
29
39
3
Mbeya City
21
10
9
2
10
39
4
Simba SC
21
9
9
3
17
36
5
Kagera Sugar
21
8
8
5
3
32
6
Ruvu Shooting
20
7
7
6
-4
28
7
Coastal Union
21
5
11
5
1
26
8
Mtibwa Sugar
21
6
8
7
-1
26
9
JKT Ruvu
21
8
1
12
-13
25
10
Prisons FC
20
3
10
7
-4
19
11
Mgambo JKT
20
4
6
10
-17
18
12
Ashanti United
21
4
6
11
-18
18
13
JKT Oljoro
21
2
9
10
-16
15
14
Rhino Rangers
21
2
7
12
-14
13
RATIBA MECHI:
Jumatano Machi 19
Yanga v Azam FC
Jumamosi Machi 22
JKT Ruvu v Mbeya City
Rhino Rangers v Yanga
Kagera Sugar v Tanzania Prisons
Jumapili Machi 23
Simba v Coastal Union
Mgambo JKT v Mtibwa Sugar
Ruvu Shooting v Ashanti United
Azam FC v JKT Oljoro