Wachezaji
31 wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20
(Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake
zitafanyika mwakani nchini Senegal.

Kikosi
kinachounda timu hiyo ambayo itarudiana na Kenya kati ya Aprili 25-27 mwaka huu
jijini Dar es Salaam kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji walioonekana katika
mpango wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke),
Manyika Peter Manyika (Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende,
Zanzibar).
Mabeki
wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union), Edward Charles (JKT Ruvu), Frank
Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel Gadiel Michael (Azam), Hussein Mkongo
(Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed (Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni
Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato
Ngonyani (Majimaji).
Viungo
ni Ally Nassoro (Coastal Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa (Azam),
Hamid Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed
Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti United), Mohamed Issa Juma
(Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin (Scouting- Kinondoni), Seleman
Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John (Scouting- Mwanza).
Washambuliaji
ni Ally Salum Kabunda (Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto,
Zanzibar), Jafari Mwambusi (Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal
(Mlale JKT), Salum Abdilah Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania
Prisons).