Sunday, February 23, 2014

VPL:SIMBA HOI YALALA TAIFA 3-2 MBELE YA JKT RUVU,AZAM YATOA SARE NA PRISON


Baada ya Jana Mabingwa Watetezi wa VPL, Ligi Kuu VodacomTanzania Bara,Yanga  Sc Kuishindilia Ruvu Shooting Kipigo Bao 7-0 na kukamata uongozi wa Ligi hiyo.
Hii leo Mambo yamegeuka kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa wapinzani wao wa Jadi Simba Wekundu wa Msimbazi imekubali kipigo cha Bao 3-2 kutoka kwa Maafande wa Jkt Ruvu.
Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na Mshambuliaji wake Mahiri Hamis Tambwe katika dakika ya 65 baada ya Kiemba kuangushwa katika eneo la hatari na muamuzi kuamuru mkwaju wa penalt.
Lakini mkali huyo alirejea tena wavuni kwa mara ya pili kunako dakika ya 84 baada kupekea krosi safi ya amri kiemba na kufunga bao hilo kwa njia ya kichwa.
Kwa upande wa Jkt Ruvu mabo yamepatikana katika dakika ya 13 mfungaji Hussein Bunu pamoja na Emmanuel Swita aliefunga magoli mawili kunako dakika ya 45 kwa njia ya penalt huku akiweka bao jingine katika dakika ya 53 baada ya kugongeana na Amos Mgisa.
Na huko kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Azam FC ikishuka kupepetana na Tanzania Prisons ya Mbeya matokeo azam imelazimishwa sare ya mabao 2-2.
Ligi Kuu Vodacom
RATIBA:
Jumapili Februari 23
Simba 2 v JKT Ruvu 3
Azam FC 2 v Tanzania Prisons 2
Jumatano Februari 26
Azam FC v Ashanti United
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Yanga SC
17
11
5
1
29
38
2
Azam FC
17
10
6
0
21
37
3
Mbeya City
19
9
8
2
8
35
4
Simba SC
19
8
8
2
19
32
5
Kagera Sugar
19
6
8
5
1
26
6
Coastal Union
19
5
10
4
5
25
7
Mtibwa Sugar
19
6
7
6
0
25
8
Ruvu Shooting
18
6
7
5
-4
25
9
JKT Ruvu
18
6
1
11
-14
19
10
Prisons FC
17
3
7
6
-5
18
11
Mgambo JKT
19
4
5
10
-17
17
12
Ashanti United
18
3
5
10
-15
14
13
JKT Oljoro
19
2
8
9
-15
14
14
Rhino Rangers
19
2
7
10
-11
13

UEFA EURO 2016: DROO KUPANGA MAKUNDI YAWEKWA HADHARANI.

DROO ya kupanga Makundi kwa ajili ya Mechi za Mchujo za kufuzu kucheza Fainali za UEFA EURO 2016, ambayo ndio Mashindano ya Mataifa ya Ulaya ,imefanyika Leo huko Palais des Congrès Acropolis Mjini Nice, France..
MAKUNDI: 
KUNDI A: Netherlands, Czech Republic, Turkey, Latvia, Iceland, Kazakhstan.
KUNDI B: Bosnia-Hercegovina, Belgium, Israel, Wales, Cyprus, Andorra.
KUNDI C: Spain, Ukraine, Slovakia, Belarus, FYR Macedonia, Luxembourg.
KUNDI D: Germany, Republic of Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar.
KUNDI E: England, Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino.
KUNDI F: Greece, Hungary, Romania, Finland, Northern Ireland, Faroe Islands.
KUNDI G: Russia, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein.
KUNDI H: Italy, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta.
KUNDI I: Portugal, Denmark, Serbia, Armenia, Albania.
EURO2016-FRANCE_LOGOMechi za Makundi zitaanza kati ya Septemba 7 na 9 Mwaka huu.
Timu mbili za juu toka kila Kundi pamoja na Timu moja Bora iliyoshika Nafasi ya 3 kwenye Makundi zitatinga Fainali na Timu 8 zilizobaki ambazo zitamaliza Nafasi ya Tatu zitapangiwa Mechi maalum za Mchujo ili kupata Timu 4 za mwisho kuingia Fainali.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 2014 hadi Oktoba 2015 na Ratiba kamili itatolewa na UEFA baada ya Droo.
Fainali za UEFA EURO 2016 zitachezwa Nchini Ufaransa kuanzia Juni 10, 2016 hadi Julai 10, 2016 na kwa mara ya kwanza Fainali hizo zitakuwa na Nchi 24 badala ya zile 16 za kawaida.
Kwa mara ya kwanza, UEFA imebuni Mtindo wanaouita ‘Wiki ya Soka’ ambao utafanya Gemu zichezwe kuanzia Alhamisi hadi Jumanne.
Saa za Mechi kuanza ni 18.00CET na 20.45CET kwa Jumamosi na Jumapili na 20.45CET kwa Alhamisi, Ijumaa, Jumatatu na Jumanne.
CET ni Saa za Ulaya ya Kati ambazo ni Masaa mawili nyuma ya Saa za Bongo kwa Majira ya Sasa.
Pia, Mtindo huo wa ‘Wiki ya Soka’ utakuwa na Wiki maalum ambapo Mechi mbili zitachezwa mfululizo, yaani Alhamisi/Jumapili, Ijumaa/Jumatatu au Jumamosi/Jumanne.
Droo kwa ajili ya Mechi za Fainali itafanyika Mjini Paris hapo Desemba 12, 2015.