Sunday, February 23, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207WATOTO WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA ANOLD ZAKAYO (06) MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA SHULE YA MSINGI MWANYANJE NA SELINA EMMANUEL (06) MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI MWANYANJE WALIFARIKI DUNIA WAKIWA WANAOGELEA KWENYE MADIMBWI YA MAJI KATIKA MTAA WA NSALAGA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI HUKO UYOLE KATA YA NSALAGA TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA VIFO HIVYO NI BAADA YA MAREHEMU HAO KUZIDIWA NA MAJI AMBAYO YAMETOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA PINDI WANAOGELEA NA WATOTO WENZAO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA/KUFUKIA/KUZIBA MITARO/VISIMA/MASHIMO YALIYO WAZI KWANI NI HATARI KWA WATOTO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA JITOKEZA.
MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG  SONGWE MKOA WA MBEYA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA SHAMBANI KWAKE.
MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG SONGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARIA LEONARD (38) MKAZI WA IGIDA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA KWENYE SHAMBA LAKE LA MAHINDI. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGIDA, KATA YA UTENGULE USONGWE, TARAFA YA SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. AWALI MNAMO TAREHE 15.02.2014 MAREHEMU ALIWAAGA WAUMINI NA MAJIRANI KUWA ANAKWENDA KUHUDHURIA MAZISHI KATIKA KIJIJI CHA ISUNGO WILAYA YA MBOZI NA TOKEA HAPO MAREHEMU HAKUONEKANA NYUMBANI MPAKA MAITI YAKE ILIPOONEKANA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UMESHAHARIBIKA HUKU PEMBENI KUKIWA NA JEMBE LAKE. TAARIFA ZA AWALI ZINASEMA HUENDA MAREHEMU ALIPIGWA NA RADI WAKATI AKIWA SHAMBANI KWAKE. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA KUKAA/KUJIFICHA KARIBU NA MITI MIKUBWA WAKATI MVUA INANYESHA KWANI NI HATARI.
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].