Saturday, February 15, 2014

VPL: MBEYA CITY YATOKA SARE 1-1 VS SIMBA DIMBANI SOKOINE

VPL_2013-2014-FPLigi Kuu Vodacom tanzania Bara  imeendelea leo katika Viwanja mbalimbali lakini mchakamchaka ulikuwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya ambapo Wagonga Nyondo Mbeya City waliumana uso kwa uso na Simba na matokeo kuwa Sare ya Bao 1-1.
Mbeya City ndio walikuwa wa kwanza kutikisa Nyavu  katika Dakika ya 14 kwa Penati ya Deogratius Julius na Amisi Tambwe kuisawazishia Simba katika Dakika ya 50.
Simba na Mbeya City sasa zimecheza Mechi mbili zaidi ya Vinara Azam FC, wenye Pointi 36, na Timu ya Pili Yanga, wenye Pointi 35.
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 15
Rhino Rangers 1 Mgambo JKT 1
Ashanti United 0 Kagera Sugar 0
Mtibwa Sugar 0 Tanzania Prisons 1
JKT Oljoro 0 JKT Ruvu 0
Mbeya City 1 Simba 1
Ruvu Shooting 1 Coastal Union 0
­­MSIMAMO  VPL:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
19
36
2
Yanga SC
16
10
5
1
22
35
3
Mbeya City
18
9
8
1
10
35
4
Simba SC
18
8
8
2
17
32
5
Ruvu Shooting
17
6
7
4
3
25
6
Kagera Sugar
18
5
8
5
0
23
7
Coastal Union
18
4
10
4
3
22
8
Mtibwa Sugar
18
5
7
6
-1
22
9
JKT Ruvu
17
6
1
10
-8
19
10
Ashanti United
17
3
5
9
-14
14
11
JKT Oljoro
18
2
8
8
-14
14
11
Mgambo
18
3
5
10
-18
14
14
Prisons FC
15
2
7
6
-9
13
12
Rhino Rangers
18 3 6 9 -10 13

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Februari 19
Tanzania Prisons v JKT Ruvu
Jumamosi Februari 22
Ruvu Shooting v Yanga
Kagera Sugar v Rhino Rangers
Mtibwa Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Mbeya City
JKT Oljoro v Mgambo JKT
Azam FC v Tanzania Prisons
Jumapili Februari 23
Simba v JKT Ruvu

FA CUP: LEO JUMAMOSI NI MAN CITY v CHELSEA!!

FA_CUP_2013-2014FA CUP
Raundi ya Tano
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 15
15:45 Sunderland v Southampton
18:00 Cardiff v Wigan
18:00 Sheff Wed v Charlton
20:15 Man City v Chelsea
Jumapili Februari 16
16:30 Everton v Swansea
18:00 Sheff Utd v Nottm Forest
19:00 Arsenal v Liverpool
Jumatatu Februari 17
22:45 Brighton v Hull City

MANCHESTER CITY v CHELSEA
Kuelekea Mechi ya leo Tunakumbuka Wiki ziliyopita, kwenye Mechi ya Ligi iliyochezwa Etihad, Chelsea waliifunga Man City Bao 1-0 na kwenye FA CUP wameshakutana mara 4 na City kufungwa mara ya kwanza, Mwaka 1915, lakini wameshinda mara zote 3 zilizobakia ikiwemo mara ya mwisho Msimu uliopita walipoifunga Chelsea 2-1 kwenye Nusu Fainali.
Man City hawajashinda katika Mechi zao mbili zilizopita, wakifungwa moja na Sare moja, lakini Chelsea hawajafungwa katika Mechi zao 12 zilizopita wakishinda 9 na Sare 3.

ARSENAL VS LIVERPOOL KESHO FEB16
Hapa kazi ipo itakuwa  FA CUP yenye upinzani kutokana Arsenal watataka kulipa kisasi cha Jumamosi iliyopita kunyukwa Bao 5-1 huko Anfield kwenye Mechi ya Ligi.
Kwenye FA CUP, Timu hizi zimekuwa zikukutana kila Msimu katika Misimu 12 iliyopita na Arsenal kushinda mara 7, zikiwemo Fainali 2, na Liverpool  kushinda Fainali 1 na kusonga mara 4 mbele ya Arsenal.
Katika Mechi za FA CUP 8 zilizopita , Arsenal wamefungwa moja tu na Liverpool na hiyo ilikuwa kwenye Fainali ya 2001.
Katika Mechi 12 zilizopita wakicheza kwao Emirates, Arsenal hawajafungwa hata Bao moja kati Mechi 11.
Liverpool hawajafungwa katika Mechi 9 zilizopita wakishinda 7 na Sare 2.

JK: MTANDAO WA UJANGILI WAJULIKANA


Rais Jakaya Kikwete, amesema mtandao wa majangili unajulikana na jitihada za serikali zimefanikiwa kukamata vigogo 40 walio kwenye mtandao mkubwa wa biashara ya nyara hizo za serikali.
 
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC , jana asubuhi alisema watuhumiwa hao wamebainika kuwa wanajihusisha na mtandao kwenye ukanda wa Kaskazini na kwamba tajiri mkuu wa biashara hiyo naye amefahamika na kwamba anapatikana mkoani Arusha .
Akizungumza katika kipindi cha Amka na BBC , alikozungumzia ujangili, alieleza kuwa mtandao umefahamika na kwamba unahusisha matajiri na miongoni mwa watu hao 40 yupo tajiri huyo wa Arusha ambaye hakutaka kumtaja jina redioni.

“Tumeutambua mtandao huo hadi wakubwa zao ni matajari pale Arusha kuna mmoja mkubwa ambaye sitaki kumtaja jina alikuwa akiendesha biashara hiyo naye yupo kwenye kundi hili la watu 40 kazi iliyokuwa ikifanyika ni kuutambua huo mtandao kwa upana,” alisema.

Awali alisema Tanzania ilikuwa na tembo wengi barani Afrika na hata duniani wakati huo baada ya Uhuru walikuwa 350,000 na ilipofikia mwaka 1987 walipungua hadi 55,000.
Alisema hapo ndipo serikali ilipofanya maamuzi ya kuingiza jeshi katika mapambano ya kupambana na ujangili jambo lililosaidia kwa kiasi kupunguza tatizo.

Hata hivyo, alisema ilipofikia mwaka 1989 shirika linaloshughulikia haki za wanyama walioko hatarini kutoweka (CITES) ilifanya maamuzi ya ku
piga marufuku biashara ya pembe za ndovu duniani.
Rais Kikwete alisema kwa mambo hayo mawili ikiwamo nguvu ya jeshi kuingilia kupambana na ujangili pamoja na biashara hiyo kupigwa marufuku duniani ilisaidia kupungua ujangili na tembo kuanza kuonekana.

Alisema ilipofika mwaka 2009 hesabu ilikuwa kubwa ambapo idadi ya tembo iliongezeka na kufikia 110,000.

Alipohojiwa juu ya gazeti moja la Uingereza la Daily Maili kumuandika kuwa hajafanya jitihada za kutosha kupambana na ujangili, alisema gazeti hilo limeandika uongo na kwamba serikali imejitahidi kufanya mikakati mbalimbali kuokoa maisha ya tembo na kupunguza ujangili.

Pembe hizo za ndovu wanaouliwa Afrika soko lake lipo katika nchi za Asia ikiwamo China.

Kikwete alisema jitihada mbalimbali zimefanywa ndiyo maana mtandao huo ambao unajihusisha na biashara ya meno ya tembo umegundulika.

Wakati Rais akiwa kwenye mkutano nchini Uingereza uliokuwa ukijadili ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na pembe za faru, polisi mkoani Singida wamemkamata George James na vipande 21 vya meno hayo.

Polisi ilisema meno hayo yenye thamani ya Sh. milio
ni 43 yana uzito wa kilo 49.

MAHOJIANO NA CNN
Wakati huo huo, ujangili umemfikisha Rais Kikwete, kwenye televisheni y
a CNN ya Marekani, alikohojiwa akitakiwa kueleza vita dhidi ya majangili inayofanyika nchini.
Akihojiwa na CNN jijini London juzi, alisema Tanzania imefanya operesheni nyingi dhidi ya majangili na kuhimiza haja ya mataifa makubwa kusaidia juhudi za kupambana na ujangili huo.
Akijibu maswali ya Christiane Amanpour wa CNN, Rais alitaka dunia kuungana kusimamisha biashara ya pembe za ndovu.

Alieleza kuwa hatua hiyo itaondoa kichocheo cha mtu kuwaua wanyama hao
Alieleza kuwa wakati wa uhuru walikuwepo tembo 350,000 kabla ya kuibuka wimbi la ujangili mkubwa ulioiachia nchi tembo 13,000 pekee.

AHADI YA MSAADA 
Akijibu swali kama kuna ahadi yoyote aliipata katika mkutano juu ya ulinzi wa wanyama pori uliofanyika London juzi, Rais Kikwete aliitaja Canada kuwa imeahidi kutoa Dola milioni mbili, wakati serikali ya Uingereza imeahidi kutoa msaada.

ALICHOTARAJIA
Alieleza kuwa kitu muhimu kwake na viongozi wa Afrika ni kufahamisha kuwa ili kuupiga vita ujangili kunahitajika rasilimali watu, kuwajengea uwezo askari wa wanyama pori wa kulinda wanyama.
Rais alisema alikuwa anategemea nchi zilizoendelea hasa Uingereza na Marekani kusaidia upande wa mafunzo ya askari wa wanyama pori na pia kuwapatia vifaa.

Alitaja silaha, magari na vyombo vyenye uwezo wa kufanya uchunguzi na kwamba ndicho alichotegemea kutoka kwenye mkutano huo na kwamba amepata ahadi za msaada.
AKIBA YA MENO
Rais Kikwete alisema Tanzania ina karibu tani 112 za pembe za ndovu ambazo haijajua itazifanya nini kwa sababu nchi ilizoea kuomba idhini ya kuziuza hatua ambayo inahitaji kuangaliwa upya.

UMASKINI
Akijibu swali kuhusu kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa kulinganisha na nchi nyingine katika kipindi cha miaka michache iliyopita lakini nchi ikiwa na maskini wanaoishi kwenye ufukara, alisema “uchumi unakua kwa asilimia 70 lakini umasikini unapungua kwa asilimia 2.0” akiongeza kuwa mchango huo wa ukuaji wa asilimia 7.0 umetokana na sekta ya mawasiliano na usafiri.  
Chanzo: Nipashe

YANGA KUTUPA KARATA LEO VS KOMOROZINE.


YANGA SC Mabingwa wa Tanzania Bara, jioni ya leo wanashuka dimbani kucheza mechi yao ya mwisho ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Komorozine mjini Moroni.
Katika me

chi ya kwanza Yanga SC walishinda mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Wacomoro Dar es Salaam Jumapili na leo wanatakiwa kumalizia vyema kazi yao dhidi ya timu hiyo dhaifu.
Endapo Yanga SC itafanikiwa kukamilisha vyema matokeo ya Randi ya Awali, basi itakutana na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misiri katika Raundi ya Kwanza. 

BALOTELI AIPA MILAN BAO LA DAKIKA ZA LALA SALAMA

Kunako dakika za  lala salama Mario Balotelli amefanikiwa kuipatia AC Milan ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bologna katika mchezo wa Serie A usiku wa jana.
Balotelli alifunga bao lake  la 10 msimu huu kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho na kuipandisha Milan hadi nafasi ya 10 ikifikisha pointi 32 sawa na Lazio iliyo nafasi ya tisa.
SERIE A
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Februari 14
AC Milan 1 Bologna 0
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 15
2245 ACF Fiorentina v Inter Milan
Jumapili Februari 16
1430 Calcio Catania v SS Lazio
1700 Atalanta BC v Parma FC
1700 Juventus FC v AC Chievo Verona
1700 Cagliari Calcio v AS Livorno Calcio

1700 Genoa CFC v  Udinese Calcio
1700 US Sassuolo Calcio v SSC Napoli
2245 AS Roma v UC Sampdoria
Jumatatu Februari 17
2245 Hellas Verona FC v Torino FC
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Juventus FC 23 19 3 1 56 18 38 60
2 AS Roma 22 15 6 1 45 11 34 51
3 SSC Napoli 23 14 5 4 47 27 20 47
4 ACF Fiorentina 23 13 5 5 42 24 18 44
5 Inter Milan 23 9 9 5 40 27 13 36
6 Hellas Verona 23 11 3 9 39 37 2 36
7 Torino FC 23 8 9 6 36 30 6 33
8 Parma FC 22 8 9 5 32 27 5 33
9 AC Milan 24 8 8 8 37 35 2 32

TWIGA STARS YA TANZANIA YALALA 2-1 ZAMBIA

Twiga Stars imepoteza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Zambia (Shepolopolo) kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.

Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga timu hizo zilikuwa suluhu.

Wenyeji ndiyo walianza kupata bao lililofungwa na Hellen Mubanga dakika ya 75. Mfungaji huyo aliyeingia kipindi cha pili nchini alimalizia wavuni mpira uliotemwa na kipa Fatuma Omari.

Dakika nne baadaye Zambia ambao walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na washabiki wao baada ya kufunga la kwanza, walipata bao la pili ambalo nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili alijifunga mwenyewe.

Mwasikili alikuwa akijaribu kutoa nje mpira uliopigwa na nahodha wa Shepolopolo, Mupopo Kabange ambapo ulipishana na kipa Fatuma Omari kabla ya kujaa wavuni.

Bao la Twiga Stars lilifungwa na Donisia Daniel dakika ya 90. Beki huyo wa kushoto ambaye pia ni mchezaji wa Tanzanite alipanda mbele kuongeza mashambulizi ambapo akiwa nje ya eneo la hatari alipiga shuti lililomshinda kipa Hazel Nali.

Akizungumza baada ya mechi, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage alisema amebaini upungufu katika kikosi chake ambao ataufanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano ili timu yake iweze kusonga mbele.

“Kwa matokeo haya bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano nyumbani na kusonga mbele,” alisema Kaijage.

Twiga Stars iliwakilishwa na Fatuma Omari, Fatuma Bashiru, Donisia Daniel, Fatuma Issa, Evelyn Sekikubo, Sophia Mwasikili, Vumilia Maarifa, Mwapewa Mtumwa/Amina Ali, Asha Rashid, Etoe Mlenzi/Zena Khamis na Shelida Boniface.

Timu hiyo inarejea nyumbani kesho kwa ndege ya Fastjet ambapo itatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
+260 976375482
Lusaka, Zambia