Mabao ya mshambuliaji huyo wa Poland yameipa Dortmund kujiweka katika nafasi nzuri ya kutingaa fainali ya klabu za bundasliga pekee itakayopigwa Uwanja wa Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern Munich kuichapa 4-0 Barcelona nchini Ujerumani pia.
Lewandowski alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
Lakini lewandowski akaonyesha makali yake katika kipindi cha pili na kufunga mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na 67 kwa penalti.
Kocha wa Real, Mreno Jose Mourinho ambaye hakutegemea kipigo hicho kitakatifu, sasa real madrid inatakiwa kutengeneza mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku Dortmund.
UCL-NUSU FAINALI
RATIBA:
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Aprili 30
Real Madrid v Borussia Dortmund [1-4]
Jumatano Mei 1
Barcelona v Bayern Munich [0-4]
FAINALI
25 Mei 2013