Mwenyekiti wa Young Africans Bw Yusuf Manji akiongea na wanachama, wazee na waandishi wa habari leo makuu ya klabu ya Yanga

Mwenyekiti
wa Young Africans Bw Yusuf Manji amesema kuondoka kwa wachezaji wao
wawili Didier Kavumbagu na Frank Domayo sio mwisho wa timu ya Yanga,
kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya kuhakikisha inasajli
wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye msimu ujao kwa
kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, Manji
amesema yameongelewa mengi sana kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao
hakuwepo nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi lakini sasa amerejea na
maandalizi ya msimu ujao yameshaanza.
Kuondoka kwa Kavumbagu ni
kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji wageni
kwa msimu mpya, huku Domayo ambae tangu mwaka jana aliombwa kuongeza
mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya
hivyo.
Pamoja na kuondoka kwa
wachezaji hao bado kwa kushirikiana na kocha Hans watahakikisha Yanga
inaendelea kutisha msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya
kimataifa, Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga
siku alipokua akiiongea na waandishi wa habari kuwaaga.

Aidha
Manji amelifuta rasmi tawi la Tandale kutokana na kuwa na chanzo cha
vurugu na migogoro ndani ya klabu, pia amewafuta uanachama wanachama
sita ambao walikiuka katiba ya Yanga kwa kwenda kuongea na waandishi na
HABARI bila ya Idhini ya uongozi huku pia wakishindwa kulipia ada zao za
uanachama kwa zaidi ya miezi sita,
waliofutwa uanachama ni:
1.
Ally Kamtande, 2. Isiaka Dude, 3. Hamisi Matandula, 4.Waziri Jitu
Ramadhani, 5.Mohamed Kigali Ndimba , 6. Selaman Hassan Migali
Mkutano
mkuu wa mabadiliko ya katiba utafanyika terehe mosi Juni, 2014 katika
Ukumbi wa Oysterbay Police Mess na wanachama wote wanaombwa kulipia ada
zao ili waweze kuhuhudhira mkutano huo wakiwa hai.
Suala la
ujenzi wa Uwanja wa Kisasa eneo la Jangwani bado lipo pale pale, kikubwa
kinachosubirwa ni majibu ya serikali juu ya maombi ya eneo la ziada,
kwani Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alisema suala hilo lipo ukingoni na
mda si mrefu.