Saturday, January 3, 2015

MAPINDUZI CUP: YANGA SC YAUWA MSUVA NYOTA YAZIDI KUPETA HETITRIKI!

Watoto wa Jangwani Yanga Sc imeanza vyema kwa kishindo cha aina yake katika Mashindano ya Mapinduzi Cup 2015 huko Visiwani Zanzibar walipoichapa Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar Bao 4-0 katika Mechi ya Kundi A huku Simon Msuva akipiga Bao 3.
Bao jingine la Yanga lilifungwa na Kpah Sherman kutoka Liberia.
Katika Mechi zilizotangulia hii Leo, KMKM na Mtende zilitoka 0-0 na Azam FC kutoka pia Sare ya 2-2 na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, KCCA ya Uganda.
MAKUNDI
KUNDI A
-Yanga
-Taifa ya Jang’ombe [Zanzibar]
-Shaba [Pemba]
-Polisi [Zanzibar]
KUNDI B
-KCCA [Uganda]
-Azam FC
-KMKM [Zanzibar]
-Mtende [Zanzibar]
KUNDI C
-Simba
-Mtibwa Sugar
-JKU [Zanzibar]
-Mafunzo [Zanzibar]
RATIBA/MATOKEO:
Saa za Bongo
Mechi zote kuchezwa Uwanja wa Amaan isipokuwa inapotajwa
Alhamisi Januari 1
JKU 2 Mafunzo 0
Polisi 1 Shaba 0
Simba 0 Mtibwa 1
Ijumaa Januari 2
KMKM 0 Mtende 0
KCCA 2 Azam FC 2
Yanga 4 Taifa ya Jang’ombe 0
Jumamosi Januari 3
3:00 JKU v Mtibwa
5:00 Mafunzo v Simba
Jumapili Januari 4
1500 KCCA v Mtende
1700 KMKM v Azam FC
1500 Taifa ya Jang’ombe v Shaba [Uwanja wa Mao]
2015 Yanga v Polisi
Jumatatu Januari 5
1500 Mtibwa v Mafunzo
2015 Simba v JKU
Jumanne Januari 6
1500 KCCA v KMKM
1500 Polisi v Taifa ya Jang’ombe [Uwanja wa Mao]
1700 Azam FC v Mtende
2015 Yanga v Shaba
Jumatano Januari 7
Robo Fainali
Mshindi Kundi C v Mshindi wa 3 Bora Na. 2
Mshindi wa Pili Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi C
Alhamisi Januari 8
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A
Mshindi Kundi A v Mshindi wa 3 Bora Na. 1
Jumamosi Januari 10
Nusu Fainali
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 2
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 4
Jumanne Januari 13
Fainali