Thursday, May 8, 2014

MABADILIKO YA KATIBA YANGA SC JUNI MOSI MWAKA HUU

Uongozi wa klabu ya Young Africans Sports Club umeitisha mkutano mkuu wa wanachama wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi kwenye baadhi ya vipengele vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi.
yanga logoAkiongea na waandishi wa habari makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani, Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha mkutano huo wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama wapate fursa ya kupitisha baadhi ya vipengele kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
“Tumekua na mawasiliano na TFF juu ya kuongezwa baadhi ya vipengele kwenye Katiba yetu kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi, baada ya hapo ni nafasi kwa wanachama wa Yanga sasa kukutana na kuweza kupitisha hivyo vipengele vitakavyoongezwa kwenye Katiba Mpya” alisema Beno.
Aidha Beno amesema wanachama wakishapitisha/kukubaliana juu ya hivyo vipengele ndipo uoungozi utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo ikishayabariki, yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua tayari ni Katiba halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.
“Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa mabadiliko juni mosi 2014  ili waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea kuwa na Katiba Mpya itakayotumika kwa  shughuli za kila siku za klabu ya Yanga SC” aliongea Beno. 
Eneo na Ukumbi utakapofanyika mkutano huo Juni Mosi 2014 utatangazwa hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika. Chanzo: Tovuti ya Yanga

PLUIJM ABWAGA MANYANGA YANGA SC, ATIMKIA HUKO UARABUNI

KOCHA  mkuu wa Young Africans, Mholanzi, Hans Van der Pluijm amepata kazi mpya nchini Saudi Arabia na tayari ameshaaga rasmi mchana huu kwa wachezaji wake, viongozi, wapenzi na wanachama wa klabu hiyo.
Pluijm aliyejiunga na Yanga mapema januari mwaka huu umepata shavu hilo katika klabu ya Al Shoalah FC inayoshiriki ligi kuu soka nchini Saudi Arabia.
SAM_2259Mholanzi huyo amemaliza mkataba wake wa miezi sita na klabu ya Yanga, lakini mbaya zaidi ameshindwa kuwasaidia wanajangwani kutetea ubingwa wao msimu huu uliomalizika aprili 19 mwaka huu. 
Yanga chini ya Pluijm ilimaliza katika nafasi ya pili, huku Azam fc chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog wakibeba taji lao la kwanza tangu wapande ligi kuu msimu wa 2008/2009. 
Pluijm alirithi mikoba ya mholanzi mwenzake, Ernie Brandts aliyetimuliwa mwezi desemba mwaka jana baada ya kufungwa mabao 3-1 na Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe.

KOMBE LA DUNIA:MWEZI UJAO JUNE 12 KUANZA KUTIMUA VUMBI

RATIBA-Mechi za Ufunguzi:
[Saa za Bongo]
Alhamisi 12 Juni 2014
KUNDI A
2300 Brazil V Croatia
Ijumaa 13 Juni 2014
1900 Mexico V Cameroon
WORLD_CUP-GROUPS

FIFA LISTI UBORA DUNIANI: SPAIN 1, BRAZIL YAKWEA HADI YA 4 TZ PALEPALE 122

Shirikisho la Soka Duniani FIFA leo limetangaza Listi ya Ubora Duniani kwa Nchi Wanachama na Mabingwa wa Dunia, Spain, wamebakiNambari Wani na Tanzania pia kubaki Nafasi yao ile ile ya 122 huku Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Juni 12, Brazil, wakipanda Nafasi 2 na kushika Nafasi ya 4.
Kukosekana kwa Mechi nyingi za Kimataifa zinazotambuliwa na FIFA, zikichezwa 13 tu, kumefanya Listi hii mpya isiwe na mabadiliko makubwa na Nchi 143 kubakia Nafasi zao zilezile za Mwezi uliopita.
TANZANIA-Walipo na Nchi zilizo karibu yao:
122    Malawi {Chini 1}
122    Tanzania {Palepale}
124    Guatemala {Palepale}
125    Burundi {Palepale}
Nchi ya Afrika ambayo iko juu sana ni Ivory Coast ambao wako Nafasi ya 21 ambayo pia waliishika Mwezi uliopita na inayofuata ni Egypt walio Nafasi ya 24 kama Mwezi Aprili.
Listi nyingine ya Ubora itatolewa Juni 5.
20 BORA:
[Kwenye Mabano Mabadiliko toka Listi ya Aprili]
1        Spain  [Wamebaki walipo]
2        Germany [Palepale]
3        Portugal [Palepale]
4        Brazil  [Juu Nafasi2]
FIFA_LOGO_BEST5        Colombia [Chini 1]
6        Uruguay [Chini 1]
7        Argentina [Chini 1]
8        Switzerland [Palepale]
9        Italy [Palepale]
10      Greece [Palepale]
11      England [Palepale]
12      Belgium [Palepale]
13      Chile [Juu Nafasi 1]
14      USA [Chini Nafasi 2]
15      Netherlands [Palepale]

16      France [Palepale]
17      Ukraine [Palepale]
18      Russia [Palepale]
19      Mexico[Palepale]
20      Croatia [Palepale]

FLYING EAGLES NDANI YA BONGO KUIVAA NGORONGORO HEROES KIINGILIO BUKU 2/=

Timu ya Nigeria (Flying Eagles) imewasili nchini kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) itakayochezwa Jumapili (Mei 11 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Flying Eagles yenye msafara wa watu 32 imewasili leo (Mei 8 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya Ethiopian Airlines ambapo imefikia hoteli ya Sapphire. Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itafanyika kuanzia saa 10 kamili
jioni.
Nigeria inayofundishwa na kocha Manu Garba itafanya mazoezi leo (Mei 8 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi siku ya Jumapili.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa ni sh. 5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza iliitoa Kenya kwa jumla ya mabao 4-3 inaendelea kujinoa jijini Dar es Salaam chini ya Kocha wake John Simkoko na Msaidizi wake Mohamed Ayoub kujiweka sawa kwa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na washabiki wa mpira wa miguu nchini.
Nigeria kama ilivyo kwa nchi nyingine 12 imeanzia moja kwa moja raundi ya pili kutokana na ratiba iliyopangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Nchi hizo ni Afrika Kusini, Angola, Benin, Burkina Faso, Cameroon, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mali, Misri, Morocco na Zambia.
MICHUANO YA BEACH SOOCER YAINGIA ROBO FAINALI
Michuano ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach soccer) inayoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikishirikisha vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam imeingia hatua ya robo fainali.
Robo fainali hiyo inayoshirikisha timu nane itachezwa Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mik
ocheni kuanzia saa 5 asubuhi, huku Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii (SWI) zikicheza robo fainali ya kwanza.
Chuo Kikuu cha Ardhi (AU) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere watcaheza robo fainali ya pili kuanzia saa 6 kamili. Saa 8 kamili itaanza robo fainali ya tatu itakayozikutanisha Taasisi ya Uhasibu (TIA) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Robo fainali ya mwisho itakayoanza saa 9 kamili itakuwa kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Utumishi Magogoni. Washindi watacheza nusu fainali Jumapili (Mei 11 mwaka huu) kwenye ufukwe huo huo.
Mechi za kutafuta mshindi wa tatu, na ile ya fainali zitachezwa kwenye ufukwe huo huo wikiendi ya Mei 17 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)