Monday, January 5, 2015

MENEJA WA LIVERPOOL ASEMA HENDERSON NDIYE MRITHI WA VIATU VYA GERRARD.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amempigia chapuo Jordan Henderson kuziba nafasi ya Steven Gerrard wakati nahodha huyo wa timu hiyo atakapoondoka mwishoni msimu huu. 
Gerrard mwenye umri wa miaka 34 amethibitisha Ijumaa iliyopita kuwa hataongeza mkataba mwingine na ataondoka katika majira ya kiangazi huku akihusishwa na kwenda kucheza soka Marekani. 
Henderson amekuwa akionyesha kiwango kizuri chini Rodgers akicheza sambamba na Gerrard na maneja huyo anaamini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ataw
eza kuziba vyema nafasi ya mkongwe huyo atapoondoka.
Akihojiwa Rodgers amesema anadhani Henderson ana haiba ya uongozi na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kumpatia unahodha msaidizi na pindi Gerrard atakapoondoka anadhani atakuja kuwa kiongozi mzuri kutokana na uzoefu aliopata.