Tuesday, April 23, 2013

KOCHA KIM ATANGAZA YOUNG TAIFA STARS
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.

Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.

“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.

Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta (Simba).

Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).

AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon na JKT Ruvu.

Mechi hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari Kambangwa, Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
VAN MAGOLI JEZI 20 APIGA TATU NA KUILETEA UBINGWA WA 20 MAN U:
Katika mechi ya jana Robin van Persie, amefanya kile ambacho wadau na mashabiki wa man u ambao waliondoa imani naye kuwa haufumanii nyavu lakini aliweza kudhihilisha kuwa yeye ni bora zaidi baada ya kutupia Bao Dakika za 2, 13 na 33 na, kufuatia kazi nzuri ya Nguli Ryan Giggs na Wayne Rooney, na kuwatwanga Aston Villa Bao 3-0 Uwanjani Old Trafford na kuipatia Manchester United Ubingwa wa BPL, Barclays Premier League huku wakiwa na Mechi 4 mkononi.
HISTORIA:
.Hii ni mara ya 4 kwa Man United kutwaa Ubingwa Uwanjani kwao Old Trafford
.Mara nyingine walizotwaa Ubingwa Old Trafford ni Mwaka 1999, 2002 na 2009
.Mwaka 2001 walitwaa Ubingwa wakiwa na Mechi 5 mkononi
.Msimu wa 1999/2000 walitwaa Ubingwa kwa pengo la Pointi 18
kwa sasa Van Persie  anaongoza Ufungaji Bora BPL akiwa na Bao 24 kwa mtukutu Luis suarez akiwa na mabao 23.
Huu ni Ubngwa wa 13, chini ya Sir Alex Ferguson, katika Miaka 21 ya Historia ya Ligi Kuu England.
MSIMAMO==BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
34
40
84
2
Man City
33
29
68
3
Arsenal
34
30
63
4
Chelsea
33
31
62
5
Tottenham
33
17
61
6
Everton
34
13
56
7
Liverpool
34
19
51
8
West Brom
33
-1
45
9
Swansea
33
1
42
10
West Ham
34
-7
42
11
Fulham
34
-8
40
12
Southampton
34
-7
39
13
Norwich
34
-20
38
14
Sunderland
34
-7
37
15
Stoke
34
-11
37
16
Newcastle
34
-17
37
17
Aston Villa
34
-27
34
18
Wigan
33
-23
31
19
QPR
34
-27
24
20
Reading
34
-28

24

PFA KUMPA USHAURI MZEE WA MENO
CHAMA cha Wanasoka wa Kulipwa-PFA kimesema kuwa mshambuliaji nyota wa Liverpool, Luis Suarez atapatiwa ushauri wa namna ya kuzikabili hasira zake kufuatia tukio lake la kumg’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay tayari ameshamuomba radhi Ivanovic kwa tukio hilo alilofanya katika mchezo wa ligi baina ya timu hizo ambao uliisha kwa sare ya mabao 2-2 lakini klabu yake imeshamtoza faini na kunauwezekano mkubwa FA nao wakatoa adhabu baadae. Suarez mwenye umri wa miaka 26 alifungiwa kucheza mechi saba baada ya kufanya tukio kama hilo wakati akiwa katika klabu ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi kipindi cha nyuma ambapo alimng’ata Otman Bakkal wa PSV. Nyota huyo asiyetabirika pia alishawahi kufungiwa mechi nane katika Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United. Ofisa Mkuu wa PFA Gordon Taylor amesema hakuna shaka juu ya kiwango bora alichonacho nyota huyo lakini inasikitisha kwa vitendo vya ambavyo amekuwa akivifanya ndio maana wameamua kumsaidia ili aweze kuzikabili hasira zake.