Nyota Mahiri Duniani Cristiano Ronaldo Jana Usiku Aliiwezesha Real Madrid
kutingaFainali ya Copa del Rey baada ya kuibwaga Atletico Madrid kwenye
Mechi ya Marudiano ya Nusu Fainali iliyochezwa Estadio Vicente
Calderon.
Penati hizo za Ronaldo zilipatikana katika Dakika
ya 7 na 16 na kuwabwaga nje Atletico Madrid ambao ndio walikuwa
Mabingwa Wateteza wa Kombe hili.
hivyo basi Real wametinga Fainali kwa Jumla ya Bao 5-0 baada kushinda Mechi ya Kwanza 3-0 huko Santiago Bernabeu Wiki iliyopita.
Kwenye Fainali Real itacheza na Mshindi
wa Leo kati ya Real Sociedad na Barcelona ambao wanarudiana huko Estadio
Anoeta huku Barcelona wako mbele kwa Bao 2-0 walizopata huko Nou Camp
Wiki iliyopita.
COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Marudiano
Jumanne Februari 11
Atletico de Madrid 0 Real Madrid CF 2 [0-5] [Estadio Vicente Calderon]
Jumatano Februari 12
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [0-2] [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19
Real Madrid v Real Sociedad/Barcelona