Wednesday, February 12, 2014

REAL MADRID KUISUBIRI MSHINDI KATI YA REAL SOCIEDAD v BARCELONA LEO:

Nyota Mahiri Duniani Cristiano Ronaldo Jana Usiku Aliiwezesha Real Madrid kutingaFainali ya Copa del Rey baada ya kuibwaga Atletico Madrid  kwenye Mechi ya Marudiano ya Nusu Fainali iliyochezwa Estadio Vicente Calderon.
Penati hizo za Ronaldo zilipatikana katika Dakika ya 7 na 16 na kuwabwaga nje Atletico Madrid ambao ndio walikuwa Mabingwa Wateteza wa Kombe hili.
hivyo basi Real wametinga Fainali kwa Jumla ya Bao 5-0 baada kushinda Mechi ya Kwanza 3-0 huko Santiago Bernabeu Wiki iliyopita.
Kwenye Fainali Real itacheza na Mshindi wa Leo kati ya Real Sociedad na Barcelona ambao wanarudiana huko Estadio Anoeta huku Barcelona wako mbele kwa Bao 2-0 walizopata huko Nou Camp Wiki iliyopita.
COPA_DEL_REY-FP
COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Marudiano
Jumanne Februari 11
Atletico de Madrid 0 Real Madrid CF 2 [0-5] [Estadio Vicente Calderon]
Jumatano Februari 12
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [0-2] [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19
Real Madrid v Real Sociedad/Barcelona