Wednesday, February 12, 2014

RIPOTI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA WAKAZI WA PWANI UKANDA WA PWANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI:


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI 
         MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700
Barua pepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: Tanzania Meteorological Agency - Admin -

S.L.P. 3056
DAR ES SALAAM
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622

10 Februari, 2014

Taarifa kwa Umma: Matarajio ya kuwa naVipindi vya Mvua kubwa, Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa.
Taarifa Na.
201402-01
Muda wa Kutolewa: Saa za Afrika Mashariki
Saa 11 Jioni
Daraja la Taarifa:
Tahadhari
Kuanzia: Tarehe
11 Februari, 2014
Mpaka: Tarehe
13 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
1. Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24)
2. Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa
pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0
Kiwango cha uhakika:
Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa
kuathirika
1. Vipindi vya Mvua Kubwa: Ukanda wa pwani mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya
Unguja na Pemba, Mbeya , Njombe, Ruvuma pamoja na kusini
mwa mkoa wa Morogoro
2. Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa: Pwani ya mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FOBANE” kusini
magharibi mwa Bahari ya Hindi. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka Pwani ya Somalia na misitu ya Congo kuelekea maeneo ya nchi yetu.
Angalizo:
Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo pale itakapobidi