Friday, August 15, 2014

SIMBA SC YA DAR YATUA VISIWANI ZANZIBAR KUWEKA KAMBI



Simba sc baada ya kumnasa kocha Mzambia Patrick Phiri na kusaini Mkataba wa mwaka mmoja jana, kikosi cha Simba SC leo kimekwendavisiwani Zanzibar leo kuweka kambi rasmi ya kujiandaa na msimu.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu na ratiba itatoka wiki moja kabla.

Tayari SImba SC imekamilisha usajili wake na wachezaji wote walikuwa wanahudhuria mazoezi mjini Dar es Salaam.


Phiri amerejea Simba SC baada ya miaka minne tangu aondoke mwaka 2010, akirithi mikoba ya Mcroatia Zdravko Logarusic aliyetupiwa virago mwishoni mwa wiki.

Haijulikani mshahara wa Phiri utakuwa kiasi gani, lakini mara ya mwisho aliondoka Simba SC akiwa analipwa dola za Kimarekani 5,000 (zaidi ya Sh. Milioni 7.5) kwa mwezi. 

Kocha huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, aliyezaliwa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi za wana Simba ‘kutembea vifua wazi’.

Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

MBOFA YASEMA MWISHO WA KULIPA ADA YA LIGI YA WILAYA NI AGOSTI 30

Chama cha mpira wa miguu wilaya ya mbozi kinatoa taarifa kwa vilabu ambavyo bado havijalipa ada ya ligi ya wilaya kwa mwaka 2014.
Vilabu hivyo vinatakiwa kulipa ada ya shillingi laki moja na mwisho wa kulipa ada hiyo ni agosti 30 mwaka huu ambapo hakutakuwa na muda wa nyongeza tena kutokana na awali ilikuwa ni tarehe 30 mwezi wa 7 mwaka huu.
Akizungumza na mtandao huu katibu wa chama cha wilaya mbozi MBOFA Willium Mwamlima amesema hiyo ni nafasi ya pekee kwa timu zilizochelewa kufika katika ofisi za chama hicho kuchukua fomu za usajili.

CLUB 12 ZA MAVETERANI WA TZ KUCHUANA TAMASHA LA MIAKA 16 YA HOME GYM

CLUB 12 za timu za soka za maveterani zinazooundwa na nyota wa zamani wa kandanda nchini zinatarajiwa kuchuana katika michezo maalum ya Tamasha la Miaka 16 ya Home Gym, itakayofanyika Septemba 6 kwenye uwanja wa Mwenge, Dar es Salaam.
Aidha zaidi ya klabu 30 za Jogging nazo zinatarajiwa kupamba tamasha hilo ambalo litahusisha pia michezo mbalimbali ikiwamo ya netiboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Andrew Mangomango, klabu za maveterani zilizothibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo litapambwa na burudani ya muziki na shoo ya watunisha misuli, wanyanyua vitu vizito, ngumi na karateka ni Mbagala Veterani, Boko, 501, Break Point, Survey, Mwenge na Msasani.
Mangomango alizitaja nyingine kuwa ni Biafra Veterani, Meeda, Mikocheni, Mbezi, Mabenzi, Segerea na Ukonga Veterani ambazo zinaundwa na nyota wa zamani wa kandanda waliowahi kutamba na timu kama za Simba, Yanga na Taifa Stars.
Juu ya klabu za Jogging mratibu huyo alizitaja kuwa ni pamoja na Temeke Jogging, Mwananyamala, Kingungi, Amani, Magenge, Makuka, 501, Ndiyo Sisi, Wastaarab, Makutanom, Pasada, FBI, Kongowe, Oysterbay Police, Zakheem, Kwa Nyoka, Kawe Beach, Satojio, Kawe Mkwamani na nyingine.
Mangomango aliongeza kuwa baada ya michezo yote wanamichezo washiriki watajumuika pamoja kuwatembelea yatima wanaolelewa kituo cha Chakuhama kwa ajili ya kuwapeleka misaada mbalimbali.
“Ni tamasha ambalo litaambatana na michezo mbalimbali kama ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, na shoo za watunisha misuli, wanamieleka, mabondia na karateka kisha kwenda kutembelea yatima,” alisema.
Mangomango alisema mgeni rasmi wa shughuli zote hizo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi cha 501, J.B Kapumbe.
Hii ni mara ya pili kwa tamasha hilo kufanyika mwaja jana lilifanyika wakati Home Gym ikiadhimisha miaka 15 tangu kuasisiwa kwake ambapo shughuli zake kuu ni kufanyisha mazoezi na kutoa ushauri juu ya afya ya mwili.

KIUNGO WA GOR MAHIA ATUA KWA WAGOSI WA TANGA ASAINI MKATABA WA MWAKA 1.

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umeizidi kete klabu ya Simba SC baada ya kumsajili kiungo kati wa timu ya Gormahia ya nchini Kenya,Rama Saluma Mohamed aliyekuwa akiwaniwa na klabu hiyo.
Rama ametua kwenye klabu ya Coastal Union  akitokea nchini Kenya na kusaini  mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha mwaka
mmoja.

PAWASA ,MATOLA,LUNYAMILA MWAMEJA KUWAKABIRI MADRID REAL

KIKOSI maalumu cha ‘Tanzania All Stars’ kitakachoshuka dimbani kuvaana na magwiji wa Real Madrid, ‘Real Madrid Legends’ kitaingia kambini jijini Dar es salaam kujiandaa na mechi hiyo itakayopigwa uwanja wa Taifa Agosti 23 mwaka huu.
baadhi ya wachezaji hawa hapa pawasa,matola,Lunyamila,mwameja,manyika waitwa kukipiga na real madrid
Makocha maarufu nchini, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’, Fredy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wataongoza benchi la ufundi la kikosi hicho , huku Daktari wa timu akiwa ni Mwanandi Mwankemwa.