Saturday, December 6, 2014

TIMU NNE ZA TZ BARA ZAALIKWA KUSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI.

Timu nne za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC, Mtibwa Sugar FC, Simba SC na Yanga SC zimealikwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayofanyika Zanzibar Januari mwakani.
Kenyan Premier League (KPL) side AFC Leopards has for the second year in a row landed an invite to take part in the Mapinduzi Cup in January 2015.
Jumla ya timu 11 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo mwakani kama ilivyothibitishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibra (ZFA), Kassim Haji Salum katika mkutano na waandishi wa habari visiwani hapa jana Ijumaa.
Endapo klabu za Azam, Mtibwa, Simba na Yanga zitashiriki michuano hiyo, ni wazi kwamba ratiba ya VPL italazimika kupanguliwa kwa mara ya tatu msimu huu baada ya kufanyiwa marekebisho na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Agosti na Oktoba mwaka huu.
Mashindano ya Kombe la Mapinduzi hufanyika kuanzia Januari 1-12/13 kila mwaka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mapinduzi tukufu ya Zanzibar.
Ratiba ya VPL mwanzoni mwa mwaka ujao inaonesha kuwa Azam FC itawaalika Mtibwa Sugar FC kwenye Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam Januari 3, Yanga SC itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya Januari 3 huku Simba SC itaalikwa na Mgambo Shooting Stars kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Januari 4.
Salum aliweka wazi kuwa barua za mwaliko zinapaswa kujibiwa na klabu kufikia Jumatatu Desemba 15, mwaka huu na mashindano yataanza rasmi Alhamisi Januari Mosi, mwakani ambapo mbali na klabu nne za VPL, mabingwa watetezi KCCA ya Uganda pia wamealikwa.
Timu nyingine zilizoalikwa ni pamoja na mabingwa wa Zanzibar KMKM, Polisi, JKU, Mtende Rangers, Shaba FC na AFC Leopards ya Ligi Kuu ya Kenya inayonolewa na Kocha James Nandwa ikishiriki kwa mara ya pili baada ya kualikwa tena mwaka huu.
Mechi ya fainali itapigwa Uwanja wa Jumanne Januari 13  na Simba SC, ikiwa chini ya Kocha Mcroatia Zdravko Logarusic ilifungwa bao 1-0 dhidi ya KCCA katika mechi ya fainali mwaka huu

WAWA BEKI MPYA WA AZAM FC ASEMA AMEKUJA KUTENGENEZA HESHIMA NA KUJIUZA KATIKA TIMU ZA ULAYA.

Pascal Wawa Beki mpya wa kati wa Azam FC ambae anaendelea na mazoezi na kikosi hicho ameweka wazi na kusema kuwa kilichomleta Tanzania ni kutengeneza heshima yake na timu kwa ujumla.
Raia huyo wa Ivory Coast ambaye majina ya wachezaji wa Yanga, Mrisho Ngassa na Juma Kaseja ndiyo yapo kwenye akili yake kutokana na namna anavyowafahamu.
Wawa anaamini Azam ndiyo itakuwa njia yake ya kutoka kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya baada ya kushindwa kufanikisha malengo yake hayo katika klabu ya El Merreikh ya Sudan alikocheza kwa miaka minne
Wawa amesema kwanza amekuja kucheza mpira Azam kwa malengo makubwa mawili, kwanza ni kujitangaza ili nisonge mbele na kupata timu katika nchi zilizoendelea Ulaya baada ya kuona nimecheza Sudani kwa miaka minne bila mafanikio.

Pili ni kuifanya Azam ifikie malengo yaliyokusudiwa kwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa, lakini yote hayo nataka kuyakamilisha kwa vitendo kimya kimya.
Wawa aliwahi kuja Tanzania kwa vipindi tofauti, kwanza akiwa na Ivory Coast iliyoshiriki CHAN mwaka 2010 na iliyocheza Kombe la Chalenji jijini Dar es Salaam pia amekuja na El Merreikh kwa vipindi tofauti kucheza mashindano ya Kombe la Kagame. Wawa ni Muivory Coast wa tatu kutua kikosini hapo baada ya Kipre Tchetche na Kipre Bolou

MSHAMBULIAJI SAIDI BAHANUZI ATUA POLISI MOROGORO KWA MKOPO

Timu ya yanga african wazee wa jangwani imemtoa mshambuliaji Said Rashid Bahanuzi kwa mkopo katika klabu ya Polisi Morogoro.
Bahanuzi amechagua kwenda Polisi badala ya timu zote zilizokuwa zikimuhitaji, Stand United na Ruvu Shooting kwa kuwa anaamini huko ni sehemu sahihi kwenda kufufua makali yake.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amejikuta katika wakati mgumu Yanga SC, baada ya kung’ara kwa msimu mmoja tu, 2012.
Bahanuzi aliingia kwa kishindo Yanga SC akiiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame la Kagame 2012 naye pia kuwa mfungaji bora.
Baada ya hapo, Bahanuzi akaanza vizuri pia kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kabla ya kuumia katikati ya msimu na kuwa nje hadi msimu uliofuata.
Hata hivyo, tangu kuumia Bahanuzi hajaweza kurejea katika kiwango chake licha ya makocha wote aliofanya nao kazi Yanga SC baada ya Mbelgiji Tom Saintfiet kumpa nafasi.
Hao ni Waholanzi Ernie Brandts na Hans van der Pluijm pamoja na huyu wa sasa, Mbrazil Marcio Maximo. 
Tangu amejiunga Yanga SC, Said Bahanuzi amecheza mechi 48 na kufunga mabao 15, matatu kwa penalti.

WAGANDA WAMSHANGAA ZARI THE BOSS LADY KUMZIMIA DIAMOND PLATNUMZ

Diamond vs Zari
Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Uganda vimemgeuka nyota wa vipindi vya runinga na Mwanamuziki Zari ‘The Boss Lady’ kwa madai kwamba amemganda mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz.
Gazeti la udaku la Red Pepper, mitandao ya ugvision.com, bigeye.ug na mingineyo, imedai kuwa nyota huyo amemganda mwanamuziki huyo tangu alipopata upenyo wa kurekodi naye singo jijini Dar es Salaam.
Mama Diamond,Diamond na Zari
Mitandao hiyo ilimshambulia Zari kwa kumwambia kuwa kavuruga uhusiano baina ya Wema na mkali huyo wa video ya ‘Ntampata Wapi’, huku ikiponda picha ambayo Zari aliiweka mitandaoni ikimwonyesha akiwa na Diamond.
Mitandao hiyo imeponda kuwa Zari ana tabia ya kuwanadi wanaume anaotoka nao.
Zari akiwa na Tuzo za Diamond Channeo o'
Wiki tatu zilizopita Zari amekuwa bega kwa bega na mwanamuziki Diamond, baada ya kutengeneza wimbo wa pamoja katika studio za Tuddy Thomas. Zari alionekana akipiga picha kadhaa na nyota huyo kabla ya kumsindikiza katika tuzo za CHOAMVA, Afrika Kusini na baadaye kurudi naye nchini.
Diamond ambaye alinyakua tuzo tatu za Channel O 2014, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla inayoandaliwa na Zari, ijulikanayo kama ‘Zari All White Ciroc Party’, itakayofanyika Desemba 18, mwaka huu.

YANGA KUIVAA EXPRESS LEO SAA KUMI JIONI UWANJA WA TAIFA

Klabu ya soka ya Yanga, ya Jijini Dar es Salaam leo jioni  itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Soka ya The Express Kutoka nchini Uganda, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Uwanja Taifa Jijini Dar es salaam.
Yanga itapambana na The Express kama sehemu ya mchezo wa maandalizi ya kujipima nguvu kuelekea pambano la mtani jembe siku ya jumamosi tarehe 13/12/20014 dhidi ya timu ya Simba SC jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa kesho kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo anatarajiwa kukitumia kikosi chake chote kwa lengo la kutazama maendeleo ya vijana wake kabla ya mchezo wa Nani Mtani Jembe wiki ijayo.
Mpaka sasa klabu ya Young Africans imefanya usajili wa mchezaji mmoja tu Emerson De Oliveira kutoka nchini Brazil ambaye anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santana "Jaja" ambaye ameomba kuachwa kutokana na kushindwa kurejea nchini kwa masuala ya kifamilia.
Wananchama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kutoka matawi mbalimbali wanaombwa kuhudhuriwa kwa wingi uwanjani, ili kutoa hamasa ya ushindi kwa wachezaji siku ya jumamosi katika uwanja mkuu wa taifa, jijini Dar es salaam.
Yanga inashiriki ligi kuu ya Tanzania bara ikiwa inashika nafasi ya pili sawa na Azam FC kwa kulingana pointi na magoli ya kufunga na kufunga, inajaindaa pia na mzunguko wa nane wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa kombe la Shirkisho baranai Afrika mapema mwakani.

KIKOSI CHA TAIFA STARS MABORESHO CHA YAREJEA JIJINI DAR ES SALAAM.

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.
Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.
Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)