Pascal Wawa Beki mpya wa kati wa Azam FC ambae anaendelea na mazoezi na
kikosi hicho ameweka wazi na kusema kuwa kilichomleta Tanzania ni
kutengeneza heshima yake na timu kwa ujumla.
Raia huyo wa Ivory Coast ambaye majina ya wachezaji wa Yanga, Mrisho
Ngassa na Juma Kaseja ndiyo yapo kwenye akili yake kutokana na namna
anavyowafahamu.
Wawa anaamini Azam ndiyo itakuwa njia yake ya kutoka kwenda kucheza soka
la kulipwa Ulaya baada ya kushindwa kufanikisha malengo yake hayo katika klabu
ya El Merreikh ya Sudan alikocheza kwa miaka minne
Wawa amesema kwanza amekuja kucheza mpira Azam kwa malengo makubwa
mawili, kwanza ni kujitangaza ili nisonge mbele na kupata timu katika nchi
zilizoendelea Ulaya baada ya kuona nimecheza Sudani kwa miaka minne bila
mafanikio.
Pili ni kuifanya Azam ifikie malengo yaliyokusudiwa kwa kufanya vizuri
kwenye michuano ya kimataifa, lakini yote hayo nataka kuyakamilisha kwa vitendo
kimya kimya.
Wawa aliwahi kuja Tanzania kwa vipindi tofauti, kwanza akiwa na Ivory
Coast iliyoshiriki CHAN mwaka 2010 na iliyocheza Kombe la Chalenji jijini Dar
es Salaam pia amekuja na El Merreikh kwa vipindi tofauti kucheza mashindano ya
Kombe la Kagame. Wawa ni Muivory Coast wa tatu kutua kikosini hapo baada ya
Kipre Tchetche na Kipre Bolou