Timu nne za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC, Mtibwa
Sugar FC, Simba SC na Yanga SC zimealikwa kushiriki michuano ya Kombe la
Mapinduzi itakayofanyika Zanzibar Januari mwakani.
Kenyan Premier League (KPL) side AFC Leopards has for the second year in
a row landed an invite to take part in the Mapinduzi Cup in January 2015.
Jumla ya timu 11 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo mwakani kama
ilivyothibitishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibra (ZFA), Kassim Haji
Salum katika mkutano na waandishi wa habari visiwani hapa jana Ijumaa.
Endapo klabu za Azam, Mtibwa, Simba na Yanga zitashiriki michuano hiyo,
ni wazi kwamba ratiba ya VPL italazimika kupanguliwa kwa mara ya tatu msimu huu
baada ya kufanyiwa marekebisho na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Agosti na
Oktoba mwaka huu.
Mashindano ya Kombe la Mapinduzi hufanyika kuanzia Januari 1-12/13 kila
mwaka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mapinduzi tukufu ya Zanzibar.
Ratiba ya VPL mwanzoni mwa mwaka ujao inaonesha kuwa Azam FC itawaalika
Mtibwa Sugar FC kwenye Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam Januari 3, Yanga SC
itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya
Januari 3 huku Simba SC itaalikwa na Mgambo Shooting Stars kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga Januari 4.
Salum aliweka wazi kuwa barua za mwaliko zinapaswa kujibiwa na klabu
kufikia Jumatatu Desemba 15, mwaka huu na mashindano yataanza rasmi Alhamisi
Januari Mosi, mwakani ambapo mbali na klabu nne za VPL, mabingwa watetezi KCCA ya Uganda pia
wamealikwa.
Timu nyingine zilizoalikwa ni pamoja na mabingwa wa Zanzibar KMKM,
Polisi, JKU, Mtende Rangers, Shaba FC na AFC Leopards ya Ligi Kuu ya Kenya
inayonolewa na Kocha James Nandwa ikishiriki kwa mara ya pili baada ya kualikwa
tena mwaka huu.
Mechi ya fainali itapigwa Uwanja wa Jumanne Januari 13 na Simba SC, ikiwa chini ya Kocha Mcroatia
Zdravko Logarusic ilifungwa bao 1-0 dhidi ya KCCA katika mechi ya fainali mwaka
huu