Timu ya yanga african wazee wa jangwani imemtoa mshambuliaji
Said Rashid Bahanuzi kwa mkopo katika klabu ya Polisi Morogoro.
Bahanuzi amechagua kwenda
Polisi badala ya timu zote zilizokuwa zikimuhitaji, Stand United na Ruvu
Shooting kwa kuwa anaamini huko ni sehemu sahihi kwenda kufufua makali yake.
Mshambuliaji huyo wa zamani
wa Mtibwa Sugar amejikuta katika wakati mgumu Yanga SC, baada ya kung’ara kwa
msimu mmoja tu, 2012.
Bahanuzi aliingia kwa
kishindo Yanga SC akiiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kagame la Kagame 2012 naye pia kuwa mfungaji bora.
Baada ya hapo, Bahanuzi
akaanza vizuri pia kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kabla ya kuumia
katikati ya msimu na kuwa nje hadi msimu uliofuata.

Hao ni Waholanzi Ernie
Brandts na Hans van der Pluijm pamoja na huyu wa sasa, Mbrazil Marcio
Maximo.
Tangu amejiunga Yanga SC,
Said Bahanuzi amecheza mechi 48 na kufunga mabao 15, matatu kwa penalti.