Mwanariadha nyota wa Marekani, Tyson Gay amefanikiwa kufuzu kushiriki mbio za mita 200 za duniani zitakazofanyika jijini Moscow kwa kutumia muda wa sekunde 19.74 ambao ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Gay ambaye ni bingwa wa dunia wa mwaka 2007, sasa atachuana na mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt katika mbio za mita 100 na 200 kwenye mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi Agosti mwaka huu. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka aliwashinda Isiah Young aliyeshika nafasi ya pili na Curtis Mitchell alishika nafasi ya tatu. Kwa upnde wa wanawake mwanadada nyota katika mbio fupi kutoka Marekani Allyson Felix alishindwa kutamba kwenye mbio za mita 200 baada kushindwa na Kimberlyn Duncan.
Saturday, June 22, 2013
MASAU BWIRE ASEMA TUPO VIZURI MSIMU UJAO WA VPL

Timu ya soka Ruvu Shooting Maafande wa kibaha mkoani pwani chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa “Masta” wamendelea kutangaza vita kwa klabu za ligi kuu Tanzania bara msimu ujao, hususani Simba, Yanga na Azam fc.
Afisa habari wa klabu hiyo Masau Bwire akizungumza na mkali wa dimba amesema kuwa msimu ujao wa ligi kuu hakuna kulala, watapambana kufa na kupona kuhakikisha wanapata nafasi tatu za juu.
Masau amesema katika kuhakikisha wanafanikisha doto zao wameendelea kufanya vizuri katika usajili na mpaka sasa wamepata nyota watano.
Mchezaji Juma Seif Dion "Kijiko" aliyekuwa akiichezea Africon Lyon msimu uliyopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara naye amejiunga na Ruvu Shooting ya Pwani kwa mkataba wa miaka miwili.
Kijiko aliyewahi pia kukipiga Yanga, alisaini mkataba huo hivi karibuni katika ofisi za timu hiyo Mlandizi, Kibaha tayari kuitumikia kwa msimu ujao.
Wakati huo huo, uongozi wa timu hiyo ya Ruvu Shooting umetangaza kuwaacha wachezaji watano kutokana na kiwango chao cha kucheza mpira kushuka.
Aidha Masau Bwire amewataja wachezaji hao kua ni Pail Ndauka, Charles Nobart, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus Manyasi.
Kwa mujibu wa Bwire, timu hiyo tayari iko kambini kikosi cha Jeshi 832 Ruvu JKT, itaanza mazoezi rasmi siku ya Jumatatu, Juni 24 chini ya Kocha Mkuu, Charles Mkwasa.
Bwire amewataka wachezaji wote ambao kawajaripoti kambini wafike haraka kabla ya Jumatatu ikiwa ni pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.
BLANC AKUBALIANA NBA PARIS SAINT-GERMAIN YA FRANCE
USAIN BOLT AFUZU KUSHIRIKI MBIO ZA MITA 100 ZA DUNIA.
Usain Bolt mwanariadha nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica amefanikiwa kutinga hatua ya kushiriki mbio za mita 100 za dunia kwa kushinda michuano ya mchujo iliyofanyika nchini kwake kwa kutmia muda wa sekunde 9.94. Katika mbio hizo Bolt alianza taratibu lakini aliongeza kasi zaidi alipofikia mita 50 na kumkumpita Nickel Ashmeade na kujihakikishia nafasi ya kwenda jijini Moscow katika michuano ya dunia ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 10 mpaka 18. Mjamaica mwingine mkali katika mbio Yohan Blake yeye alishindwa kushiriki mbio za kuvuzu za mita 200 kwasababu ya majeraha lakini atashiriki mbio za mita 100 kama bingwa mtetezi baada ya Bolt kuenguliwa katika mbio hizo kwenye michuano ya dunia iliyofanyika jijini Daegu mwaka 2011. Kwa upnde wa Marekani nyota wa mbio hizo Tyson Gay naye amefanikiwa kukata tiketi ya kwenda Moscow baada ya kumshinda Justin Gatlin katika mbio za mita 100 kwa kutuimia muda wa sekunde 9.75 ukiwa ni muda wake wa haaka zaidi kwa mwaka huu.
ACCELOTT MTAZAMA ROONEY KWA JICHO LA TATU ZAIDI"
Carlo Ancelott ambaye kwa sasa ni kocha mpya wa Real Madrid, katika moja ya harakati zak ni kumsajili Wayne Rooney majira haya ya joto kama mshambuliaji huyo asiye na furaha atashindwa kumaliza tofauti zake na Manchester United.
Katika hali ya kawaida tunafahamu kabisa Rooney anapenda zaidi kuungana na Jose Mourinho ndani ya Chelsea ikiwa atamaliza miaka yake tisa ya kuishi United, lakini Madrid itakuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ikiwa ataondoka.
Klabu zote hizi mbili zina uwezo sana tu wa kulipa Pauni Milioni 30 za ada ya uhamisho wake na kumlipa mchezaji mwenyewe mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.
Kocha wa zamani wa Chelsea, Ancelotti anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mrithi wa Mourinho Jumatatu na atakabidhiwa orodha ya wachezaji wanaotakiwa, wakiwemo Rooney, Gareth Bale, Edinson Cavani na Luis Suarez.
Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake, atakuwa na mazungumzo na kocha mpya wa United, David Moyes baada ya wote kurejea baada ya wote kurejea kutoka mapumzikoni siku chache zijazo, lakini inaonekana kama atabadilisha mawazo yake juu ya kwenda kuanza maisha mapya.
Wakati huo huo, kocha wa zamani wa Ufaransa, Laurent Blanc anajiandaa kurithi mikoba ya Ancelotti ya ukocha wa Paris Saint-Germain.
Baada ya mpango wa mabingwa hao wa Ufaransa kumchukua kocha wa zamani wa England, Fabio Capello kukwama, sasa beki wa zamani wa Manchester United, Blanc, mwenye umri wa miaka 47 atapewa mikoba
Makubaliano Kati ya Laurent Blanc na Paris St Germain yamefikiwa leo yeye kuwa kocha mpya wa klabu ya Jiji hapa ni kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa.
Makubaliano baina ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na PSG yamekubaliwa kwa miaka miwili. Ilipangwa kwamba, atasaini Mkataba wiki ijayo,
Subscribe to:
Posts (Atom)