RATIBA/MATOKEO:
Jumapili
Aprili 6
Yanga
5 vs JKT Ruvu 1
Coastal
Union 0 vs Mgambo JKT 2
JKT
Oljoro 2 v Tanzania Prisons 1
Rhino
Rangers 0 v Mtibwa Sugar 1
Jumatano
Aprili 9
Ruvu
Shooting v Azam FC
MABINGWA
wa VPL-Ligi Kuu Vodacom, Yanga, Leo wameweka hai matumaini yao ya kutetea
Ubingwa wao baada ya kuitandika Ruvu JKT Bao 5-1 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaa huku Straika wao, Mrisho Ngassa, akipiga Hetitriki.
Hadi
Mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa Bao za Ngassa, Dakika ya 8 na 15, na Didier
Kavumbagu, Dakika ya 38.

Bao
pekee la Ruvu JKT lilifungwa na Iddi Mbaga katika Dakika 84.
Ushindi
huu umeifanya Yanga iwe na Pointi 49 kwa Mechi 33 na wako Nafasi ya Pili huku
Azam FC wakiendelea kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 23.
Mgambo
Shooting leo ikicheza katika mechi dhidi ya Coastal Union, imeibuka na ushindi
wa mabao 2-0, hivyo kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu
Bara.
Kabla ya
hapo, Mgambo ilizitungua Yanga na Simba kwenye uwanja huo wa Mkwakwani.
Mechi
nyingine mjini Arusha, wenyeji JKT Oljoro wamewaonyesha Prisons ‘rigwaride’
baada ya kuwachapa mabao 2-