Makocha wa timu za Tanzania (Ngorongoro Heroes), John Simkoko na Nigeria (Flying Eagles), Manu Garba wanakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati yao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.

Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 20 itafanyika Jumapili (Mei 11 mwaka huu) saa 10
kamili jioni katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.