Friday, November 21, 2014

FIFA KUPITIA KWA UHAKIKA UPYA RIPOTI YA GARCIA.


SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limethibitisha kamati yake ya ukaguzi itapitia upya taarifa yote ya mchakato wa uenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 baada ya kikao kati ya wakili Michael Garcia na jaji wa maadili Hans-Joachim Eckert. 
Taarifa ya mapitio ya ripoti ya uchunguzi wa Garcia kuhusiana na masuala ya rushwa ilitolewa na jaji Eckert wiki iliyopita huku Urusi na Qatar zikisafishwa kuwa wenyeji halali wa michuano hiyo ya mwaka 2018 na 2022. 
Jaji Eckert alikiri kuwepo matukio kadha katika ripoti hiyo lakini hayakuingilia mchakato wa kutafuta wenyeji katika michuano hiyo. 
Haraka taarifa hiyo iliyokuwa na kurasa 42 ilipingwa vikali na wakili Garcia alioongoza uchunguzi huo kwa miaka miwili akisisitiza kumekuwa na makosa kadhaa kadhaa kulinganisha na ripoti yake iliyokuwa na kurasa 430.
Jaji Eckert na Garcia alikutana ili kusawazisha mambo na kufikia uamuzi huo wa kupeleka ripoti yote kwa kamati ya ukaguzi kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi.

NDANDA YAJIWEKA FITI LIGI KUU YAJIPANGA KUSAJILI WA NGUVU.

Timu ya Ndanda FC katika kuhakikisha inatoa dozi Ligi Kuu Bara ya imeamua kusajili wachezaji kutoka Burundi na katika timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.

Ndanda inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani katika msimamo wa ligi kuu, tayari imeshaingia mkataba na kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Masoud Ally Mohamed ‘Chille’ ambaye kwa sasa anaichezea Zanzibar Heroes.

Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mashambuliaji, Indeshyme Dumu raia wa Burundi ambaye alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini Djibouti.

Selemani Kachele Katibu wa Ndanda, akizunghumza na mtandao huu amesema kuwa nia yao ni kusajili wachezaji sita wakati huu wa dirisha dogo.

Ndanda inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani katika msimamo wa ligi kuu  ikiwa na point 6, tayari imeshaingia mkataba na kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Masoud Ally Mohamed ‘Chille’ ambaye kwa sasa anaichezea Zanzibar Heroes.

Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mashambuliaji, Indeshyme Dumu raia wa Burundi ambaye alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini Djibouti.

Katibu wa Ndanda, Selemani Kachele amesema nia yao ni kusajili wachezaji sita wakati huu wa dirisha dogo.

TAARIFA KWA MASHABIKI KUHUSU KOCHA JUMA MWAMBUSI-UONGOZI.

Uongozi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya unapenda kuwaarifu mashabiki na wadau wa Timu ya Mbeya City Fc kuwa suala lililojitokeza wiki iliyopita kuhusiana na kocha mkuu wa timu hii Juma Mwambusi kujiuzulu, litatolewa maelezo na ufafanuzi wiki ijayo.
Hivyo basi mashabiki na wadau wa timu ya Mbeya City Fc  mnaombwa  kutulia mpaka  ufafanuzi  au taarifa  rasmi juu ya jambo hili itakapotolewa, pia  mashabiki mnaombwa kuwa makini na baadhi ya watu ambao wanataka kutumia mwanya huu  kuzusha  chokochoko nyingi kwa lengo la kuleta mgawanyiko na kuvuruga umoja wetu.
Kwa sasa Juma Mwambusi bado ni mwalimu wa Mbeya City Football Club{Vikao vya ndani vinaendelea kuhusu suala hili}.

MKUSANYIKO WA U12 DAR ES SALAAM

Watoto wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.

Mkusanyiko wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

Wachezaji hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MPANGO WAFANYIKA KULIPA MAMA WANAONYOSHA WATOTO.

Matokeo ya awali ya mpango wa kulipa wanawake ili kuwashawishi kunyonyesha watoto umeonesha matokeo mazuri, watafiti wameeleza.
Wakina mama katika maeneo matatu ya Derbyshire,South Yorkshire ambapo kiwango cha unyonyehsaji kiko chini kati ya asilimia 21 mpaka 29 waliahidiwa kulipwa mpaka pauni 200.
Kati ya wanawake 108 walio katika mpango huu,wanawake 37 sawa na asilimia 34 tayari wamelipwa katika kipindi cha wiki sita mpaka nane.
Wakosoaji wakiwemo madaktari wanasema mradi huu unachochea uwepo wa vitendo vya rushwa.
Mpango mwingine utafuata ambao utakua mkubwa zaidi utakaowahusisha wanawake 4,000
Tayari Wanawake 58 wamejiandikisha.
Nchini Uingereza, asilimia 51 ya wanawake kwa kipindi cha wiki sita mpaka nane, scotland kwa asilimia 38.
Takwimu ziko chini zaidi kwenye maeneo yaliyo masikini mpka kwa kiasi cha asilimia 12.
Wataalamu wa afya wanasema watoto wanatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita, ili kuwalinda watoto dhidi ya maradhi.
Halikadhalika tafiti zinasema kuwa kunyonyesha mtoto kunamuepusha mzazi kupata maradhi ya saratani ya matiti na Ovari.
lakini hali haiko hivyo nchini Uingereza ikilinganishwa na nchi nyingine, asilimia moja tu ya watoto nchini humo hunyonya maziwa ya mama zao kwa miezi sita.

RONALDO DILIMA AOSHA VYOMBO BAAADA YA KUSHINDWA.

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda fedha hizo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula