Saturday, May 24, 2014

MBEYA CITY YAANZA VYEMA YAITANDIKA ACADEMI YA BURUNDI 3-MTUNGI

IMG_1150
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea nchini Sudan , Mbeya City fc  wameanza kutupa karata yao ya kwanza vyema hii leo majira ya 11:30 jioni kwa saa za Sudan dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.

Ambapo katika mchezo huo mbeya city imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 3-2 mabao hayo yakiwekwa kimiani na  Paul nonga,kaptein Mwagane yeya pamoja Themi felix katika mechi hiiyo iliopigwa uwanja wa Al-Merreikh mjini Khartoum
.

TP MAZEMBE SAMATA, ULIMWENGU DHIDI YA AS VITA MJINI LUBUMBASHI

1WASHAMBULIAJI  wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samata na Thomas Emmanuel Ulimwengu kesho jumapili wanatarajia kuiongoza TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya wapinzani wao wakubwa, AS Vita mjini Lubumbashi.
Timu hizi hasimu zitakutana katika mchezo wa kesho zikiwa na kumbukumbu ya kusababisha maafa ya vifo vya watu zaidi ya 15 katika mchezo wao wa ligi kuu ya DR Congo wiki za karibuni.
Tukio hilo baya lilitokea mjini Kinshasa baada ya mashabiki wa AS Vita kutoridhishwa na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzania wao TP Mazembe.
Mchezo wa kesho umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka, kwani timu hizi zinapokutana, upinzani unakuwabmkubwa mno nje ya uwanja na ndani ya uwanja.

FAINALI BEACH SOCCER KUTIMUA VUMBI KESSHO JUMAPILI

Fainali ya michuano ya mpira wa miguu ya ufukweni (beach soccer) kati ya timu za Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) inachezwa kesho (Mei 25 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
beach-soccer-finalTimu hizo zimepata nafasi ya kucheza fainali baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali dhidi Chuo Kikuu cha Ardhi (AU) na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) zilizochezwa wikiendi iliyopita.
Mgeni rasmi katika fainali hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Azam Tv atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na itaanza saa 4.15 asubuhi. Fainali hiyo itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya AU na TIA kuanzia saa 3 kamili asubuhi.
Michuano hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini ilishirikisha vyuo 13 vya Dar es Salaam, na ilianza Aprili 20 mwaka huu katika fukwe za Escape One na Gorilla iliyopo Kigamboni.
Vyuo vingine vilivyoshiriki ni Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ).
Tanzania itashiriki katika michuano ya Afrika ya mpira wa miguu wa ufukweni itakayofanyika mwakani nchini Shelisheli                                                                        
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

STARS KUPASHA MISULI NA MALAWI JUMANNE KABLA YA KWENDA ZIMBABWE

10357474_634079413340945_8148690486284095511_nTaifa Stars na Malawi (Flames) zinapambana Jumanne (Mei 27 mwaka huu) katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni.
Mechi hiyoakuwa ya mwisho kwa Taifa Stars kujipima kabla ya kucheza mchezo wa marudiano wa michuano ya Afrika na Zimbabwe (Mighty Warriors) utakaofanyika Juni Mosi mwaka huu jijini Harare.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya chini ya Kocha wake Mart Nooij kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi na ile ya Zimbabwe.
                                                                       Na Boniface Wambura, Dar es salaam