Wednesday, July 9, 2014

STARS, MSUMBIJI KIINGILIO 7,000/=, TIKETI KWA M-PESA.

TFF-MPESA-MALIPOKiingilio cha chini cha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 7,000.
Tiketi zinapatikana kwa mfumo wa elektroniki kupitia M-PESA. Kiingilio hicho kwa ajili ya viti vya rangi ya rangi ya chungwa, kijani na bluu. Viingilio katika maeneo mengine vitatangazwa baadaye.
TFF-TANZANIA-MSUMBIJIMshabiki ili apate tiketi anatakiwa kutumia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, ingiza namba ya kampuni 173399 kisha weka 7000 kwenye namba ya kumbukumbu ya malipo, na weka
7000 kama kiasi cha bei ya tiketi na mwisho weka namba yao ya siri.
Baada ya hapo utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo kwa ajili ya kuchukulia tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.
TFF-MPESAVituo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illutions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).
Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na ofisi za TFF (PPF Tower).
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

VPL:LIGI KUU KUANZA SEPTEMBA 20


Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2014/2015 itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.
VPL_2013-2014-FPAwali michuano hiyo ilikuwa ianze Agosti 24 mwaka huu, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limelazimika kuisogeza mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupitisha michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Michuano ya Kombe la Kagame inayoshirikisha mabingwa wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itafanyika Agosti mwaka huu nchini Rwanda.
Timu 14 zitashiriki Ligi Kuu msimu huu. Timu hizo ni mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Polisi Morogoro, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons na Yanga.
Ratiba ya ligi hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)