Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa
2014/2015 itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.

Michuano ya Kombe la Kagame
inayoshirikisha mabingwa wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira
wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itafanyika Agosti mwaka huu
nchini Rwanda.
Timu 14 zitashiriki Ligi Kuu msimu huu.
Timu hizo ni mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars,
Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC,
Polisi Morogoro, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons na
Yanga.
Ratiba ya ligi hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)