CLUB ya Simba sc wazee wa Msimbazi wamefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa
Coastal Union Abdi Banda baada ya kumuweka kwenye rada zake kwa muda mrefu.
Banda aliwahi kuripotiwa
kuwindwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwaka huu, lakini
ilishindikana kwasababu alikuwa na mkataba na wagosi wa kaya na viongozi wa
klabu hiyo walilalamika kitendo cha wanajangwani kumrubuni kijana huyo.