Tuesday, February 18, 2014

WATANO WALALAMIKIWA KAMATI YA MAADILI, MMOJA KUHUSU OKWI!

TFF_LOGO12Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewalalamikia wana familia watano wa mpira wa miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na udanganyifu katika mtihani wa utimamu wa mwili wa waamuzi na usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi.

 Riziki Majala na Army Sentimea ambao ni wakufunzi wa waamuzi, na Oden Mbaga na Samwel Mpenzu ambao ni waamuzi wanadaiwa kughushi nyaraka kuhalalisha mtihani huo kinyume cha taratibu.

Naye Sabri Mtulla analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.
Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo.
TWIGA STARS, ZAMBIA KUCHEZA MACHI 2
Mechi ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) itachezwa Machi 2 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Twiga Stars tayari imeingia kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.
Shepolopolo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.
Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.
TWIGA_STARS_MATUMAINIWachezaji wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mustafa, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
STAND UNITED YAIKATIA RUFANI KANEMBWA JKT
Stand United ya Shinyanga imekata rufani Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikipinga Kanembwa JKT ya Kigoma kuchezesha wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo kwenye mechi ya kiporo iliyozikutanisha timu hizo.
Mechi hiyo namba 22 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilichezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Kanembwa JKT iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika rufani yake, Stand United inadai kwenye mechi hiyo Kanembwa JKT ilichezesha wachezaji wanane waliosajiliwa katika dirisha kidogo kinyume na maelekezo kutoka TFF kwa timu hizo kuwa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo hawawezi kucheza mechi hiyo.
Wachezaji wanaodaiwa kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi hiyo ni Hamidu Juma, Ibrahim Shaban Issa, Joseph Mlary, Lucas Charles Karanga, Raji Ismail, Salvatory Kulia Raphael, Seif Ibrahim Zaid na Yonathan David Sabugowiga.
Dirisha dogo lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka jana, hivyo Stand United katika rufani yake inaombwa ipewe pointi tatu na mabao matatu kwa Kanembwa JKT kuchezesha wachezaji wasiostahili.
Awali mechi hiyo ilichezwa Novemba 2 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, na kuvunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya Kanembwa JKT kugomea pigo la penalti dhidi yao.
RAIS MALINZI AENDA KUJITAMBUSHA CAF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameondoka leo (Februari 17 mwaka huu) kwenye Cairo, Misri kujitambulisha kwa uongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Akiwa Cairo, Rais Malinzi ambaye alichaguliwa Oktoba 28 mwaka jana atakutana na Rais wa CAF, Issa Hayatou pamoja na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Hicham El Amrani.
WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA
Wachezaji watatu wanaocheza mpira wa miguu nchini Tanzania wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.
Mchezaji Khamis Mroki Jamal aliyekuwa na timu ya Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam ameombewa ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.
Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa Tanzania itatoa ITC hizo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

UCL-KAZI IPO MTOTO HATUMWI DUKANI MAN CITY VS FC-ETIHAD

 BIGI Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, leo Jumanne Februari 18 mechi kali kati ya Manchester City na Barcelona itakayo pigwa katiaka dimba la Etihad ambapo Mechi nyingine ni  kati ya Bayer Leverkusen na Paris Saint-Germain.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]

Jumanne Februari 18
22:45 Manchester City v FC Barcelona
22:45 Bayer 04 Leverkusen v Paris Saint-Germain
BAYER 04 LEVERKUSEN v PARIS SAINT-GERMAIN
Bayer Leverkusen hawategemewi kuifunga Paris Saint-Germain kwenye Mechi hii lakini Meneja wao Sami Hyypia hakubali hilo.
Hyypia, ambae alitwaa Ubingwa wa UCL Mwaka 2005 akiichezea Liverpool, anakiri kuwa Klabu Tajiri PSG ndio ambao wanategemewa kusonga kwenda Robo Fainali kwa sababu ya kuwa na Vipaji vingi na vya bei ghali lakini yeye anaamini Kikosi chake ni madhubuti kama Timu.
Amesema: “Lazima tucheze mwisho wa kikomo chetu na kujituma Asilimia 100. Nguvu yetu ni umoja wetu kama Timu!’’
UCL_2013_LOGO
Kwa Upande wa Meneja wa PSG, Nguli wa France, Laurent Blanc, ataweza kuisimamia Timu yake toka Benchi la Ufundi baada ya UEFA kusitisha Kifungo chake cha Mechi moja ambayo alipewa kama Adhabu baada ya Timu yao kupewa onyo mara mbili kwa kuchelewa kuingia Uwanjani kwa ajili ya Mechi zao za Hatua ya Makundi ya UCL na ilipotokea mara ya 3 ndipo Adhabu ikatolewa na kusitishwa ili kuwekwa kwenye ulinzi maalum.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP

VPL:KESHO PRISON KUTUPA KARATA YAKE VS JKT RUVU

UWANJA wa Sokoine huko Jijini Mbeya, Kesho unatarajiwa kuchukua Nafasi kwa pambano la VPL, Ligi Kuu Vodacom, ambapo Wenyeji Tanzania Prison wakishuka dimbani kuvaana  na Jkt Ruvu Kutoka Kibaha Mkoani pwani.VPL_2013-2014-FP
Tanzania Prison watashuka dimbani kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu ili Kujiweka mahala Pazuri kuepuka Janga la kushaka daraja.
a,mbapo kwa sasa Katika msimamo wa VPL Prison ipo Nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na Alama 13 huku mpinzani wake akiwa katika Nafasi ya 9 na alama 19a Magoli.
­­

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
19
36
2
Yanga SC
16
10
5
1
22
35
3
Mbeya City
18
9
8
1
10
35
4
Simba SC
18
8
8
2
17
32
5
Ruvu Shooting
17
6
7
4
3
25
6
Kagera Sugar
18
5
8
5
0
23
7
Coastal Union
18
4
10
4
3
22
8
Mtibwa Sugar
18
5
7
6
-1
22
9
JKT Ruvu
17
6
1
10
-8
19
10
Ashanti United
17
3
5
9
-14
14
11
JKT Oljoro
18
2
8
8
-14
14
11
Mgambo
18
3
5
10
-18
14
14
Prisons FC
15
2
7
6
-9
13
12
Rhino Rangers
18
3
6
9
-10
13

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Februari 19
Tanzania Prisons v JKT Ruvu
Jumamosi Februari 22
Ruvu Shooting v Yanga
Kagera Sugar v Rhino Rangers
Mtibwa Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Mbeya City
JKT Oljoro v Mgambo JKT
Azam FC v Tanzania Prisons
Jumapili Februari 23
Simba v JKT Ruvu

KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII AKEMEA DAWA ZA KULEVYA

KATIBU Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Anna Maembe ametaka vijana vijana nchini kuachana kabisa na biashara ya dawa za kulevya kwani inawasababishia matatizo makubwa katika maisha yao badala yake wajiunge na kutengeneza vikundi vya kijasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kujikwamua kimaisha na kufikia ndoto zao.
Katibu Mkuu Anna Maembe akisalimiana na akina mama wanakikundi cha kutunza Mazingira katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa jana. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMA
Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa, zaidi ya vijana 500 wa Kitanzania wako kizuizini katika nchini tofauti duniani walikokamatwa wakisafirisha dawa hizo, huku vijana wengine wapatao 100 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa nchini China.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii wakati wa ziara yake katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa jana, ambapo alisema biashara hiyo inachafua sana jina la Tanzania katika Jumuia ya Kimataifa kutokana na idadi kubwa ya vijana kujihusisha na biashara hiyo.
Akizungumzia sera ya Jinsia inayotekelezwa na wizara yake, Katibu Mkuu huyo alisema haina lengo la kuwafanya wanawake kuwatunishia misuli wanaume katika familia bali ni kuwawezesha wanawake kushiriki katika uzalisha na kukuza kipato cha familia na taifa  kwa ujumla ili kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimepanda sana kwa sasa.
Vilevile alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto ili kujua changamoto zinazowakabili ikiwemo unyanyasaji wa kijinsi na kisaikolojia wanazokumbana nazo na pia kuwapatia haki zao za kimsingi kama elimu, afya na kusikilizwa kama  ambavyo sera ya watoto hapa nchini inavyoelekeza.
Katika kuimarisha vikundi vya wanawake mkoani Rukwa, katibu mkuu Maembe ametoa shilingi milioni 43 kutoka katika wizara yake, ambapo vikundi kutoka katika Halmashauri za wilaya ya Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Vijijini na Manispaa vitanufaika kwa mtindo wa wanachama wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo kwa ajili ya kutekeleza shughuli zao za kiuchumi.
                                 Na Ramadhani Juma,
                   Afisa Habari Ofisi ya Mkurugenzi -Kalambo

LOGARUSIC NITAFANYA KWELI MSIMBAZI KUHUSU WACHEZAJI"L

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema matokeo mabaya ya timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara ambayo iko hatua ya lala salama yanatokana na kuwa na baadhi ya wachezaji wasio na viwango 'mizigo'.

Logarusic alisema ili kikosi chake kiweze kurejea katika ushindani atawatema kwenye programu zake wachezaji hao ambao amewakuta wameshasajiliwa.

Hata hivyo, kocha huyo raia wa Croatia, hakuwa tayari kuwataja majina nyota hao wanaomwangusha katika mechi za ligi na kusababisha timu yao kuendelea kukaa kwenye nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu.

Baadhi ya wachezaji ambao wanadaiwa wamekuwa wakifanya 'ndivyo sivyo' na kumchanganya kocha huyo ni pamoja na Betram Mwombeki, Uhuru Selemani na Zahor Pazi ambaye Jumamosi jijini Mbeya aliingia kuchuka nafasi ya Haroun Chanongo katika dakika ya 54 na kupoteza nafasi zaidi ya tatu za kuifungia Simba na kufanya mechi hiyo imalizike kwa sare ya 1-1.

Baada ya mechi ya ugenini dhidi ya Mbeya City, Logarusic, alisema kwamba ubingwa wa ligi bado uko wazi na ili Simba iweze kurejesha matumaini ya kumaliza katika nafasi za juu ni lazima mabingwa watetezi, Yanga, Azam na Mbeya City zilizoko juu yake zifanye vibaya kwenye mechi zao.

Simba yenye pointi 31 huku ikiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, jana jioni ilianza mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi, Sinza kwa ajili ya kujiandaa na mechi yake itakayofanyika Jumapili, Februari 23, mwaka huu dhidi ya JKT Ruvu.

Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia katika mashindano ya kimataifa ndio mabingwa watetezi wa ligi wakati Azam ndio vinara wakiwa na pointi 36 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 35 na Mbeya City wakiwa na pointi 34 ni watatu.