UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 18
22:45 Manchester City v FC Barcelona
22:45 Bayer 04 Leverkusen v Paris Saint-Germain
BAYER 04 LEVERKUSEN v PARIS SAINT-GERMAIN
Bayer Leverkusen hawategemewi kuifunga Paris Saint-Germain kwenye Mechi hii lakini Meneja wao Sami Hyypia hakubali hilo.
Hyypia, ambae alitwaa Ubingwa wa UCL
Mwaka 2005 akiichezea Liverpool, anakiri kuwa Klabu Tajiri PSG ndio
ambao wanategemewa kusonga kwenda Robo Fainali kwa sababu ya kuwa na
Vipaji vingi na vya bei ghali lakini yeye anaamini Kikosi chake ni
madhubuti kama Timu.
Amesema: “Lazima tucheze mwisho wa kikomo chetu na kujituma Asilimia 100. Nguvu yetu ni umoja wetu kama Timu!’’
Kwa Upande wa Meneja wa PSG, Nguli wa France,
Laurent Blanc, ataweza kuisimamia Timu yake toka Benchi la Ufundi baada
ya UEFA kusitisha Kifungo chake cha Mechi moja ambayo alipewa kama
Adhabu baada ya Timu yao kupewa onyo mara mbili kwa kuchelewa kuingia
Uwanjani kwa ajili ya Mechi zao za Hatua ya Makundi ya UCL na ilipotokea
mara ya 3 ndipo Adhabu ikatolewa na kusitishwa ili kuwekwa kwenye
ulinzi maalum.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP