VIDIC WA MAN UNITED AKUBALI KWENDA YAKE ITALY
BEKI Kisiki Nemanja Vidic wa Man united amekubali kujiunga na Inter Milan ya
Italia. Nyota huyo wa kimataifa wa Serbia ambaye alitangaza Januari
kuamua kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu anatazamiwa kuasaini
dili la mkataba wa miaka miwili ambao utamuwezesha kulipwa kitita cha euri
milioni tatu kwa mwaka. Kuna taarifa kuwa Vidic aliwafahamisha viongozi
wake wa United kuhusu uamuzi wake wa kukubali kwenda nchini Italia baada
ya kufikia makubaliano kwenye mchezo waliotoka sare ya bila ya
kufungana na Arsenal katika uwanja wa Emirates Jumatano iliyopita. Ofisa
mkuu wa Inter, Piero Ausilio amekuwa na mawasiliano ya karibu na nyota
huyo toka Januari alipotangaza kutaka kuondoka. Toka atangaze kuondoka
Vidic amekuwa akiwendwa na vilabu mbalimbali huku Monaco ya Ufaransa na
Galatasaray ya Uturuki zikiwa mojawapo lakini nyota huyo ameamua kwenda
Italia. Vidic alijiunga na United akitokea klabu ya Spartak Moscow ya
Urusi mwaka 2006 na amefanikiwa kushinda mataji matano ya Ligi Kuu na
moja la Ligi ya Mabingwa barani ULaya katika kipindi cha miaka nane
aliyokaa Old Trafford.