WENGER AMJIBU MBWATUKAJI MOURINHO
Kocha wa Klabu ya
Arsenal, Arsene Wenger amefafanua kauli ya Jose Mourinho kumuita
mtaalamu wa kushindwa kuwa ni kauli ya kijinga na iliyokosa
heshima. Kauli ya hiyo ya Mourinho aliitoa kujibu kauli iliyotolewa na
Wenger kuwa baadhi ya mameneja wa timu za Ligi Kuu nchini Uingereza
wanadai kuwa hawana mpango na taji hilo msimu huu kutokana na uoga
wao. Akihojiwa Wenger amesema hataki kuingia katika vita ya maneno na
Mourinho lakini anadhani kauli yake ni aibu kwa timu yake ya Chelsea
kuliko ilivyo kwake. Wenger amesema asingependa kuzungumzia kauli za
kijinga na zilizokosa heshima kwasababu huwa hapendi kumzungumzia
Mourinho katika mikutano yake na waandishi wa habari na hatakuja kufanya
hivyo. Kocha huyo alikipongeza kikosi chake kwa kucheza vizuri katika
mchezo dhidi ya Liverpool ambao uliwawezesha kukata tiketi ya robo
fainali ya Kombe la FA kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.