Thursday, August 28, 2014

USAJIL LIGI KUU VODACOM TZ BARA BADO WADUNDADUNDA WAPINGWA KALENDA TENA.

Baada ya tarehe 17 baada ya hapo ukaja tarehe 27 na sasa usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa wachezaji wa ndani umesogezwa mbele kwa masaa 48 kuanzia jana, kutokana na timu kushindwa kukamilisha usajili katika muda husika jana. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Selestine Mwesigwa ambapo amesema sababu za kusogeza mbele ni klabu zote za Ligi Kuu kushindwa kukamilisha usajili jana.
Mwesingwa amesema kilichopelekea vilabu vimeshindwa kuutumia huu mfumo wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa 48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo hakuna nafasi tena, tunasonga mbele. Amesema kwamba hadi muda wa kufunga usajili jana Saa 6:00 usiku, ni timu moja ya Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake katika mfumo huo.
Mwesingwa amesema tff inapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili wao ndani ya muda. Hata hiyo Mwesigwa amesema kwamba dirisha la usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 6, mwaka huu. “Hili dirisha la wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA, likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe hawafanyi makoasa.

TWIGA STARS KUELEKEA AFRIKA KUSINI IJUMAA AGOSTI 29 MWAKA HUU.

TIMU ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya nchi hiyo (Banyana Banyana). Twiga Stars inakwenda huko kwa mwaliko wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) katika mji wa Polokwane.
Msafara wa timu hiyo utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Saloum ambapo utajumuisha wachezaji 18 na benchi la ufundi lenye watu watano.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Amina Bilali, Anastaz Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Fatuma Jawadu, Fatuma Makusanya, Fatuma Maonya, Fatuma Swaleh, Happiness Mwaipaja, Maimuna Said, Mwajuma Abdillahi,
Mwanahamis Shurua, Shelda Mafuru, Sophia Mwasikili, Therese Yona na Zena Rashid.
Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Rogasian Kaijage, na msaidizi wake Nasra Mohamed. Wengine ni Christine Luambano (daktari), Furaha Mnele (Meneja) na Mwanahamisi Nyomi (mtunza vifaa). Timu hiyo inatarajia kurejea nchini Septemba 2 mwaka huu kwa ndege ya Fastjet.

TANZANIA YAPIGWA CHINI KUANDAA UENYEJI AFCON 2017.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeliandikia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuhusiana na kipengele cha kutaka kwanza nchi iandae Fainali za Afrika kwa Vijana ndiyo iwe na sifa ya kuandaa Fainali za Afrika (AFCON) kiondolewe.
TFF ilishapeleka barua CAF kutaka kipengele hicho kiondolewe, na kutaka kijadiliwe katika Congress (Mkutano Mkuu) ujayo wa CAF.
Tanzania imeshaiandikia CAF barua kuomba uenyeji wa Fainali za AFCON za 2017 baada ya Libya iliyokuwa imepewe uenyeji huo kujitoa. Uamuzi wa Tanzania kuomba kuandaa fainali hizo ulifanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24 mwaka huu.

MTIHANI WA WAAMUZI, MAKAMISHNA KUFANYIKA SEPTEMBA 5

MTIHANI wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wanaotaka kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu utafanyika katika vituo viwili kuanzia Septemba 5-6 mwaka huu.
Waamuzi watakaoshiriki mtihani huo ni wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa class one. Pia kutakuwa na semina wa makamishna wanaotaka kusimamia mechi za VPL na FDL ambayo itafanyika Septemba 7 mwaka huu.
 

Vituo vya mtihani huo ni Dar es Salaam na Shinyanga. Kituo cha Dar es Salaam ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Kituo cha Shinyanga ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Waamuzi wote ambao wamechezesha VPL na FDL msimu wa 2013/2014 na kupata matatizo au kuondolewa kwenye ligi hawahusiki na mtihani huo. Washiriki wanatakiwa kufika kituoni siku moja kabla.
Wasimamizi ni Charles Ndagala, Israel Mujuni, Issarow Chacha, Joan Minja, Pascal Chiganga, Riziki Majala, Said Nassoro, Salum Chama, Soud Abdi,Victor
wandike na Zahara Mohamed.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameandaa kozi ya ukufunzi wa utawala itakayofanyika Desemba mwaka huu.
Kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu, ambapo sifa ya chini ya elimu kwa wanaotaka kushiriki ni kidato cha nne.
Kwa wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 5 mwaka huu ambapo wanatakiwa pia kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya kitaaluma.

MECHI ZA TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUPIGWA TANGA, BUKOBA.

Mechi nyingine ya tiketi za elektroniki siku hiyo itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuzikutanisha timu za Kagera Sugar na Geita Gold SC ya mkoani Geita. Geita Gold iko Daraja la Kwanza Kabla ya mechi hizo, Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) saa 3 asubuhi kwenye viwanja hivyo kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki pamoja na jinsi mfumo huo unavyofanya kazi. Washiriki wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa vituo vya Tanga na Bukoba, viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (KRFA) na Tanga (TRFA), makatibu na maofisa habari wa klabu za Kagera Sugar, Mgambo Shooting, African Sports na Geita Gold, mameneja wa viwanja vya Kaitaba na Mkwakwani na wasaidizi wao, maofisa usalama wa TRFA na KRFA, wachanaji tiketi, wasimamizi wa milangoni, wasaidizi (stewards) na waandishi wa habari.

RAIS TFF KUTUA MANYARA, KILIMANJARO, ARUSHA

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atatembelea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Katika ziara hiyo atakutana na viongozi na kuangalia hali hali ya mpira wa miguu katika mikoa hiyo na mahitaji yake. Pia atazungumzia maono (vision) ya TFF katika mpira wa miguu. Rais Malinzi atawasili mkoani Manyara, Agosti 29 mwaka huu, na ataanza ziara rasmi katika mkoa huo Agosti 30 mwaka huu. Agosti 31 mwaka huu atakuwa Arusha, na kumalizia Septemba 1 mkoani Kilimanjaro. Katika ziara hiyo, Rais Malinzi atafuatana na Mkurugenzi Msaidizi (Wanachama) wa TFF, Eliud Mvella. Pia Septemba 8 mwaka huu, Rais Malinzi ataanza ziara ya mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.