RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atatembelea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Katika
ziara hiyo atakutana na viongozi na kuangalia hali hali ya mpira wa
miguu katika mikoa hiyo na mahitaji yake. Pia atazungumzia maono
(vision) ya TFF katika mpira wa miguu.
Rais
Malinzi atawasili mkoani Manyara, Agosti 29 mwaka huu, na ataanza ziara
rasmi katika mkoa huo Agosti 30 mwaka huu. Agosti 31 mwaka huu atakuwa
Arusha, na kumalizia Septemba 1 mkoani Kilimanjaro.
Katika
ziara hiyo, Rais Malinzi atafuatana na Mkurugenzi Msaidizi (Wanachama)
wa TFF, Eliud Mvella. Pia Septemba 8 mwaka huu, Rais Malinzi ataanza
ziara ya mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.