Wednesday, August 27, 2014

SIMBA YAMUWEKA KUNDINI MUSOTI AMPIGA BAO BUTOYI OKWI JE.



Rais wa Simba, Evans Aveva amemaliza utata wa usajili wa wachezaji wa kigeni uliokuwa umeigubika klabu hiyo kwa kusema Mkenya Donald Mosoti ndiye anabaki na Mrundi Butoyi Hussein wamempiga chini huku Yanga nao wakimpiga chini Emmanuel Okwi raia wa Uganda.
Simba na Yanga zimelazimika kufanya uamuzi mgumu wa kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni ambao wamezidi katika klabu zao kwa sababu usajili wa wachezaji katika klabu za Ligi Kuu Bara unamalizika leo saa 6 usiku.
Mrundi huyo alimvutia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akiichezea Telecom ya Djibouti katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda mwezi huu.
Maana yake wachezaji wa kigeni katika kikosi cha Simba SC watakuwa mabeki Mganda Joseph Owino, Mkenya Mosoti, Warundi kiungo Pierre Kwizera, mshambuliaji Amisi Tambwe na Mkenya Mkenya Paul Kiongera.
Kwa upande wa Yanga ambapo nayo ilikuwa na wachezaji sita wa kigeni ambapo awali Hamis Kiiza ambaye ni raia wa Uganda ndiye aliyekuwa anadaiwa kuachwa, lakini habari za ndani kutoka katika klabu ya Yanga zinasema panga limemwangukia Emmanueli Okwi ambaye hadi jana asubuhi alikuwa hajajiunga na timu.