Akizungumza na mkali wa dimba tz.blogspot.com afisa habari wa timu hiyo jaffari iddi maganga amesema kuwa wachezaji wote wataanza mazoezi kesho, kasoro wale ambao wameitwa timu ya taifa.
Maganga amesema kwamba wachezaji
wawili, Aishi Manula na Kevin Friday japokuwa hawapo kwenye kikosi cha Taifa
Stars, wao wamepewa mapumziko zaidi- hivyo si lazima waanze kesho.
Aidha Maganga amesema kwamba Simba
SC waliomba mchezo wa kirafiki na wao wikiendi hii, lakini imeshindikana kwa
sababu kocha Joseph Marius Omog amesema hawezi kuwa na mechi baada ya mazoezi
ya siku mbili.
Mwalimu
amesema mchezo wanaotaka Simba SC labda wiki ijayo, kwa sababu hawezi kufanya
mazoezi Alhamsi na Ijumaa halafu baada ya hapo awe na mechi ngumu.
Mcamreoon huyo ambaye aliipatia azam
Ubingwa msimu uliopita hivi karibuni ameifikisha Azam FC Robo Fainali ya Kombe
la Kagame mjini Kigali kabla ya kutolewa na El Merreikh ya Sudan, iliyoibuka
bingwa wa michuano hiyo mwaka huu.
|