Wednesday, August 27, 2014

SIMBA YAIFUMUA MAFUNZO 2-0 MECHI YA KIRAFIKI

Elias Maguri mshambuliaji  mpya wa simba ameanza kufunga bao lake la kwanza baada ya Simba SC kuifumua bao 2-0 dhidi ya wenyeji Mafunzo jioni hii Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa kirafiki. Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Ruvu Shooting ya Pwani msimu huu, alifunga bao hilo la kwanza katika mchezo huo, dakika ya 60 baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Mrundi Amisi Tambwe ambapo Winga Haroun Chanongo aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 71 
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda/Hussein Sharrif ‘Cassilas’ dk80, Miraj Adam/William Lucian ‘Gallas’ dk80, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ dk80, Joram Mgeveke/Donald Mosoti dk80, Joseph Owino/Hussein Butoyi dk80, Pierre Kwizera/Said Ndemla dk42, Haroun Chanongo/Uhuru Suleiman dk80, Amri Kiemba/Abdallah Seseme dk65, Amisi Tambwe/Elias Maguri dk46, Shaaban Kisiga ‘Malone’/Ibrahim Hajibu dk80 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Twaha Ibrahim.