
Klabu ya Everton imekamilisha usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto'o.
Mshambuliaji huyo mzoefu amesaini kandarasi ya miaka miwili katika hiyo ya Goodison Park, baada ya kuitumika msimu uliopita katika klabu ya Chelsea.
QPR na majirani zao Liverpool walikuwa pia na mawazo ya kumsajili Eto'o, ambaye anaweza kupatikana katika mchezo wa Premier League siku ya Jumamosi kati yake ya Everton na timu yake ya zamani Chelsea katika uwanja wa Goodison Park.