MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea tena jana na kushuhudia timu za Barcelona, Bayern Munich, Paris Saint-Germain-PSG na FC Porto nazo zikitinga hatua ya timu 16 bora baada ya kushinda michezo yao. Katika michezo ya michuano hiyo iliyochezwa juzi mabingwa watetezi Real Madrid na Borussia Dortmund nao walitangulia katika hatua hiyo baada ya kushinda mechi zao. Barcelona wao walifanikiwa kusonga mbele baada ya kuitandika Ajax Amsterdam kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na nyota wake Lionel Messi wakati Bayern Munich wao waliichapa kwa mara nyingine AS Roma kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Allianz Arena. PSG wao walisonga mbele baada ya kuitandika Apoel kwa bao 1-0 huku Porto nao wakicharuka na kuichapa Athletic Bilbao kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na nyota wa Colombia Jackson Martinez na Mualgeria Yacine Brahimi.
Wiki hii imekuwa mbaya kwa timu za Uingereza kwani baada ya Liverpool kuiweka rehani nafasi yao ya kusonga mbele kwa kufungwa na Madrid kwa bao 1-0 huku Arsenal wakitoa sare nyumbani na Anderlecht, Chelsea nao wameingia katika mkumbo huo baada ya kugawana alama na Maribor kwa kutoka sare ya bao 1-1. Kwa upande wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu hali yao ndio imezidi kuwa mbaya baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika Uwanja wa Etihad na kuweka matumaini yao ya kusonga mbele katika mashaka.
Thursday, November 6, 2014
MESSI AFIKIA REKODI YA RAUL BAO 71 AMBWAGA RONALDO UEFA
Mshambuliaji Mahiri wa Argetina na Barcelona Lionel Messi amefanikiwa kuifikia rekodi ya nyota wa zamani wa Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Raul Gonzalenz alikuwa akishikilia rekodi ya kufunga mabao 71 na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Cristiano Ronaldo alionekana ndiye atakuwa wa kwanza kumfikia Raul,lakini mabao mawili aliyofunga Messi wakati Barcelona ikiichalaza Ajax magoli 2-0 kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, yamekwamisha ndoto za Ronaldo.
Wafungaji Bora: wa Kihistoria Uefa.
Lionel Messi: Magoli 71 Mechi 90-Barcelona.
Raul: Magoli 71 Mechi 142-Real Madrid na Shalke 04.
C'Ronaldo: Magoli 70 Mechi 107-Man united na R'Madrid
Ruud van Nistelrooy: Magoli 56 Mechi 73-Psv Eindhoven,Man U na R'Madrid.
Thierry Henry: Magoli 50 Mechi 112-Arsenal,Barca,Los angel marekani.
JESHI LA POLISI MBEYA LAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUUZA NYAMA YA MBWA
KATIKA tukio la kushangaza mwanaume mmoja amekamatwa na polisi wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kuuza nyama ya Mbwa.
Mtuhumiwa huyo amefahamika kwa jina la Ahad Jesikaka mwenye umri wa miaka 20, mkazi wa kijiji cha Ngyekye, kata ya Matema, wilayani humo.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema kuwa amewauzia kitoweo hicho watu wawili.
Amewataja walionunua nyama hiyo ni Enock Nsemwa mwenye miaka 25, na Anyandile Mbwilo mwenye umri wa miaka 29, wote wakazi wa Ngyekye.
Hata hivyo anatoa wito kwa jamii kuwa makini hususuni wanaponunua vyakula ili kujiepusha na madhara ya kiafya.
MWANAFUNZI WA DARASA LA 5 AFARIKI KWA VIBOKO NCHINI KENYA
Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya msingi ya Kiuu Kenya amefariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kufeli somo lake la Kiswahili.

Mama wa mwanafunzi huyo Grace Muthoni amesema mtoto wake alienda shule Jumatatu asubuhi na aliporudi alianza kulalamika maumivu ya kichwa na shingo, siku iliyofuatia alimpeleka Zahanati ya Wilaya ya Nyagiti level 4.
Siku ya pili alilazimika kumrudisha Hospitali baada hali yake kuzidi kuwa mbaya daktari akashauri ahamishiwe katika Zahanati ya Muran’ga Level 4 kwa matibabu zaidi wakati akisubiri gari la wagonjwa akafariki dunia.
Mama huyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtoto wake alipigwa na Mwalimu na kupata majeraha kichwani na shingoni, mwili wake umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi kubaini sababu za kifo chake.
Mwalimu anayedaiwa kumpiga Mwanafunzi huyo alikimbia kujificha shimoni baada ya kusikia taarifa za kifo, huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Joseph Mwenda akikanusha uvumi kwamba mtoto huyo alifia shuleni.
Subscribe to:
Posts (Atom)