Monday, April 29, 2013

AZAM FC WATUA MOROCO KWA MCHEZO WA MARUDIANO


CLUB ya  azam FC imefika salama nchini Morocco tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji, FAR Rabat, Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi wiki hii.  

Azam, imewasili Cassablanca, majira ya saa 9:15 za huku Alasiri, sawa na saa 10:15 za Afrika Mashariki na kusafiri kwa basi kwa saa mbili kwenda Rabat, mji ambao mechi itachezwa.

Azam imetua Morocco ikitokea Dubai, UAE ambako ilifika usiku jana saa 6:00 kwa saa za huko sawa na saa 5:00 kwa saa za Afrika Mashariki, ikitokea Dar es Salaam.
Msafara huo unaouhusisha wachezaji na benchi la Ufundi, baada ya awali viongozi na wapenzi kadhaa kutangulia nchini humo, ili kuweka mazingira sawa, uliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya shirika la Emirates, wadhamini wa Arsenal ya England saa 11:00 jioni kwa saa za Tanzania.
Ni safari ndefu iliyohusisha mabara mawili, kutoka Afrika, Tanzania kupitia Asia Dubai na kurudi Afrika nchini Morocco.
Azam walilala katika hoteli ya nyota tano ya Copthorne Dubai kabla ya kuunganisha ndege saa 7:35 asubuhi ya leo kuja Morocco kesho.
Azam imefikia katika hoteli ya Golden Tulip, maeneo ya Rabat, kaskazini mwa Cassablanca,  kilomita 120 kutoka Uwanja wa Ndege wa Cassablanca, umbali wa takriban saaa mbili.

Azam itaanza rasmi mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo, ambao wanatakiwa kutoa sare ya mabao au kushinda ili kusonga mbele, baada ya awali katika mchezo wa kwanza kulazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Azam, itakuwa Rabat kwa wiki nzima hadi Jumamosi itakapocheza mechi na imejipanga vema kuhakikisha inavuka hatua hii. 

DIMBANI UCL-NUSU FAINALI KUENDELEA LEO

MARUDIANO
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Aprili 30
Real Madrid v Borussia Dortmund [1-4]
Jumatano Mei 1
Barcelona v Bayern Munich [0-4]
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, London.

MECHI ZILIZOBAKI KWA KUTAFUTA 4 BORA LIGI KUU UINGEREZA BPL
ARSENAL-Mechi zilizobaki:
4 Mei: QPR [Ugenini]
14 Mei: Wigan [Nyumbani]
19 Mei: Newcastle [Ugenini]
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
CHELSEA-Mechi zilizobaki:
5 Mei: Man United [Ugenini]
8 Mei: Tottenham [Nyumbani]
11 Mei: Aston Villa [Ugenini]
19 Mei: Everton [Nyumbani]
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
TOTTENHAM-Mechi zilizobaki:
4 Mei: Southampton [Nyumbani]
8 Mei: Chelsea [Ugenini]
12 Mei: Stoke [Ugenini]
19 Mei: Sunderland [Nyumbani] 

MSIMAMO
NA TIMU P GD PTS
1 Man Utd 35 43 85
2 Man City 34 30 71
3 Chelsea 34 33 65
4 Arsenal 35 30 64
5 Tottenham 34 17 62
6 Everton 35 14 59
7 Liverpool 35 25 54

MAKAMU M/KITI SIMBA AIPONGEZA YANGA KUTWAA UBINGWA


KLABU ya Simba imewapongeza watani zao Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku wakiapa kuwatibulia furaha kwa kuwafunga katika mechi ya kufunga pazia la ligi hiyo itakayochezwa Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Joseph Itang’ale ikiwa ni siku chache tangu Yanga itwae ubingwa wa ligi hiyo baada ya Azam kutoka sare ya bao 1-1 na Coastal Union ya Tanga, hivyo kutokewepo timu yenye ubavu wa kuzifikia pointi 56 ilizonazo hadi sasa.
Kinesi amesema pamoja na pongezi hizo, wajiandae kwani wamejipanga kutibua furaha hiyo kwa kuwafunga na kamwe hawawezi kukubali kuvuliwa ubingwa na kufungwa na mtani wao.
Kinesi ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo anayekaimu nafasi ya Makamu Mwenyekiti baada ya kujiuzulu kwa Geofrey Nyange  amesema japo watani zao wametwa ubingwa, wasitarajie ushindi Mei 18.
 ambapo wekundu hao ndio mabingwa wa msimu uliopita baada ya kuwachalaza watani hao bao 5-0 toka ligi kuu ianzishwe simba imetwaa taji hilo mara 18 huku yanga ikitwaa mara 24
Mwaka 1965, 1966 (as Sunderland)
1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1993, 1994, 1995, 2001/02, 2002/03, 2004/05, 2007/08, 2009/10, 2011/12 
Mwaka1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011,2013

FERGUSON NASEMA LIVERPOOL WALIKUWA SAWIA SAWIA.


BOSI wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema  kuwa nakuweka imani kuwa uongozi wa Liverpool ulikuwa sahihi kutochukua hatua dhidi ya mshambuliaji wao Luis Suarez kabla ya kufungiwa mechi 10 na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kumng’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic. Ferguson amesema tukio hilo linamkumbusha jinsi walivyotendwa na FA baada ya mshambuliaji wake Eric Cantona kumpiga teke la kung-fu mshabiki wa Crystal Palace mwaka 1995. Ferguson amedai kuwa FA iliwahakikishia kuwa hatachukua hatua zaidi kama United watamuadhibu mchezaji huyo lakini pamoja na United kumfungia Cantona miezi minne, chama hicho kiliongeza adhabu na kufikia miezi nane. Kwa matokeo hayo yaliyowakuta United kipindi hicho Ferguson amesema ameelewa kwanini Liverpool hawakumuadhibu nyota huyo mapema.

GARETH BALE ATWAA UCHEZAJI BORA PFA.

KIUNGO machachali wa klabu ya Tottenham Hotspurs Gareth Bale amekuwa mchezaji wa tatu kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wakubwa na wachezaji wanaochipukia kwa msimu mmoja, tuzo ambazo hutolewa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa nchini Uingereza. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia alishinda tuzo ya wakubwa mwaka 2011, amefunga mabao 19 katika ligi msimu huu na kuwa nyuma ya kinara wa mabao Robin van Persie mwenye mabao 25 na Luis Suarez mwenye mabao 23. Akikabidhiwa tuzo hiyo Bale amesema ni heshima kubwa kwake kunyakuwa tuzo hizo mbili muhimu na kushukuru wapiga kura kwa kutambua mchango wake haswa ikizingatiwa kumekuwa na majina makubwa mengine katika orodha iliyokuwepo. Bale anaungana na wachezaji wengine walioshinda tuzo ya wakubwa mara mbili ambao ni Cristiano Ronaldo, Thierry Henry, Alan Shearer and Mark Hughes wakati walioshinda tuzo zote mbili kwa mwaka mmoja ni Ronaldo mwaka 2007 na Andy Gray mwaka 1977.


REKODI ZA BALE:


-2012-13 (Inaendelea): Mechi 29, Magoli 19, Amesaidia 4
-2011-12: Mechi 36, Magoli 9, Amesaidia 10
-2010-11: Mechi 30, Magoli 7, Amesaidia 1
-2009-10: Mechi 23, Magoli 3, Amesaidia 5
-2008-09: Mechi 16, Magoli 0, Amesaidia 0
-2007-08: Mechi 8, Magoli 2, Amesaidia 0

WASHINDI WALIOPITA:
2011-12: Gareth Bale (Tottenham)
2011-12: Robin van Persie (Arsenal)
2010-11: Gareth Bale (Tottenham)
2009-10: Wayne Rooney (Man Utd)
2008-09: Ryan Giggs (Man Utd)
2007-08: Cristiano Ronaldo (Man Utd)
Wanandinga wengine ambao walikuwa wakigombea na Bale ni 
Michael Carrick wa Man United, 
Wachezaji wa Chelsea Eden Hazard na Juan Mata, ambao wote hao pamoja na Suarez na Van Persie wapo Kwenye Timu Bora ya Mwaka ya Wachezaji 11.

Gareth Balle
Gareth Bale - Spurs vs Brighton.jpg
Kuhusu yeye
Full name Gareth Frank Bale
Date of birth 16 July 1989 (age 23)
Place of birth Cardiff, Wales
Height 1.86 m (6 ft 1 in)
Playing position Winger
Timu ya sasa
Current club Tottenham Hotspur
Number 11
Academy
2005–2006 Southampton
Timu za ukubwa
Years Team mechi (Goli)
2006–2007 Southampton 40 (5)
2007– Tottenham Hotspur 142 (40)
Timu ya taifa
2005–2006 Wales U17 7 (1)
2006 Wales U19 1 (1)
2006–2008 Wales U21 4 (2)
2006– sasa Wales 41 (11)

MATAJI
Southampton Academy 

TUZO BINAFSI