KLABU
ya Simba imewapongeza watani zao Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku
wakiapa kuwatibulia furaha kwa kuwafunga katika mechi ya kufunga pazia la ligi
hiyo itakayochezwa Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Joseph Itang’ale ikiwa
ni siku chache tangu Yanga itwae ubingwa wa ligi hiyo baada ya Azam kutoka sare
ya bao 1-1 na Coastal Union ya Tanga, hivyo kutokewepo timu yenye ubavu wa
kuzifikia pointi 56 ilizonazo hadi sasa.
Kinesi
amesema pamoja na pongezi hizo, wajiandae kwani wamejipanga kutibua furaha hiyo
kwa kuwafunga na kamwe hawawezi kukubali kuvuliwa ubingwa na kufungwa na mtani
wao.
Kinesi ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
klabu hiyo anayekaimu nafasi ya Makamu Mwenyekiti baada ya kujiuzulu kwa
Geofrey Nyange amesema japo watani zao
wametwa ubingwa, wasitarajie ushindi Mei 18.
ambapo wekundu hao ndio mabingwa wa msimu uliopita baada ya kuwachalaza watani hao bao 5-0 toka ligi kuu ianzishwe simba imetwaa taji hilo mara 18 huku yanga ikitwaa mara 24
Mwaka 1965, 1966 (as Sunderland)

Mwaka1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989,
1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009,
2011,2013