Monday, April 29, 2013

GARETH BALE ATWAA UCHEZAJI BORA PFA.

KIUNGO machachali wa klabu ya Tottenham Hotspurs Gareth Bale amekuwa mchezaji wa tatu kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wakubwa na wachezaji wanaochipukia kwa msimu mmoja, tuzo ambazo hutolewa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa nchini Uingereza. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia alishinda tuzo ya wakubwa mwaka 2011, amefunga mabao 19 katika ligi msimu huu na kuwa nyuma ya kinara wa mabao Robin van Persie mwenye mabao 25 na Luis Suarez mwenye mabao 23. Akikabidhiwa tuzo hiyo Bale amesema ni heshima kubwa kwake kunyakuwa tuzo hizo mbili muhimu na kushukuru wapiga kura kwa kutambua mchango wake haswa ikizingatiwa kumekuwa na majina makubwa mengine katika orodha iliyokuwepo. Bale anaungana na wachezaji wengine walioshinda tuzo ya wakubwa mara mbili ambao ni Cristiano Ronaldo, Thierry Henry, Alan Shearer and Mark Hughes wakati walioshinda tuzo zote mbili kwa mwaka mmoja ni Ronaldo mwaka 2007 na Andy Gray mwaka 1977.


REKODI ZA BALE:


-2012-13 (Inaendelea): Mechi 29, Magoli 19, Amesaidia 4
-2011-12: Mechi 36, Magoli 9, Amesaidia 10
-2010-11: Mechi 30, Magoli 7, Amesaidia 1
-2009-10: Mechi 23, Magoli 3, Amesaidia 5
-2008-09: Mechi 16, Magoli 0, Amesaidia 0
-2007-08: Mechi 8, Magoli 2, Amesaidia 0

WASHINDI WALIOPITA:
2011-12: Gareth Bale (Tottenham)
2011-12: Robin van Persie (Arsenal)
2010-11: Gareth Bale (Tottenham)
2009-10: Wayne Rooney (Man Utd)
2008-09: Ryan Giggs (Man Utd)
2007-08: Cristiano Ronaldo (Man Utd)
Wanandinga wengine ambao walikuwa wakigombea na Bale ni 
Michael Carrick wa Man United, 
Wachezaji wa Chelsea Eden Hazard na Juan Mata, ambao wote hao pamoja na Suarez na Van Persie wapo Kwenye Timu Bora ya Mwaka ya Wachezaji 11.

Gareth Balle
Gareth Bale - Spurs vs Brighton.jpg
Kuhusu yeye
Full name Gareth Frank Bale
Date of birth 16 July 1989 (age 23)
Place of birth Cardiff, Wales
Height 1.86 m (6 ft 1 in)
Playing position Winger
Timu ya sasa
Current club Tottenham Hotspur
Number 11
Academy
2005–2006 Southampton
Timu za ukubwa
Years Team mechi (Goli)
2006–2007 Southampton 40 (5)
2007– Tottenham Hotspur 142 (40)
Timu ya taifa
2005–2006 Wales U17 7 (1)
2006 Wales U19 1 (1)
2006–2008 Wales U21 4 (2)
2006– sasa Wales 41 (11)

MATAJI
Southampton Academy 

TUZO BINAFSI